Wakuu wa taasisi za Kiislamu nchini Uswisi wameelezea nafasi muhimu ya wafuasi wa dini hiyo tukufu nchini humo na kutaka dini ya Uislamu itambuliwe rasmi nchini Uswisi.
Muungano wa Taasisi za Kiislamu Uswisi ambao unawakilisha taasisi zote za Kiislamu nchini humo umetangaza kuwa, wataalamu wa sheria na wasomi wa vyuo vikuu wanasisitiza kwamba, hakuna kizuizi chochote cha kutambuliwa rasmi dini ya Kiislamu nchini humo.
Corinne Weber mmoja wa mawakili maarufu nchini Uswisi amesema yuko tayari kulishughulikia na kulifikisha kunakohusika ombi la Muungano wa Taasisi za Kiislamu na kusisitiza kuwa, suala hilo la kutambuliwa dini ya Kiislamu linawezekana, kwa sababu serikali ya Uswisi inaheshimu haki za wananchi wake.
Mkuu wa Muungano wa Taasisi za Kiislamu ameeleza kuwa, kutambuliwa rasmi dini ya Kiislamu itakuwa hatua muhimu ya kushirikishwa Waislamu kwenye masuala ya kijamii na kuchukua maamuzi muhimu ya nchi.
Amesema kuwa, hatua ya kutambuliwa rasmi dini ya Kiislamu itasaidia kufichuliwa makundi yenye misimamo inayouchafua Uislamu.
Chanzo": Ahbarul rasul
0 comments