Thursday, 10 April 2014

KIKWETE APATA TUZO YA UTUMISHI BORA BARANI AFRIKA.

By    
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete ametunukiwa Tuzo ya Utumishi Bora wa Umma Barani Afrika katika sherehe kubwa iliyofanyika Washington nchini Marekani.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ikulu ya Tanzania Tuzo hiyo ambayo imepokelewa, kwa niaba ya Rais Kikwete, na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernard Membe imetolewa na jarida maarufu la kimataifa la African Leadership Magazine kwa Rais Kikwete kwa kuwa "Kiongozi wa Afrika aliyetoa mchango mkubwa zaidi katika maendeleo ya kiuchumi ya wananchi wake kwa mwaka 2013."

Pamoja na Rais Kikwete, Waafrika wengine ambao wamepewa heshima kwenye sherehe hiyo ni Dkt. Kingsley Moghalu, Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Nigeria na Bwana John Kennedy Opara, Katibu Mtendaji wa Tume ya Mahujaji Wakristo wa Nigeria ambaye pia ni mshauri wa Rais Gooluck Jonathan wa nchi hiyo kuhusu mahusiano ya kidini nchini Nigeria.


Jarida la African Leadership Magazine ambalo huchapishwa mjini London, Uingereza na mjini Washington nchini Marekani, lilimchagua Rais Kikwete kushinda Tuzo hiyo kwa mwaka 2013 baada ya wasomaji na wadau wake wengine wa Jarida hilo kuwa wamemchagua kwa njia ya kura ya maoni Rais Kikwete kama kiongozi aliyetoa mchango mkubwa zaidi kwa maendeleo ya wananchi wake katika Bara la Afrika.
 


Chanzo:BBCSWAHI

0 comments