Na Lucas Kulwa wa Wapenda SOKA (Kandanda)
EPL Sura 38:2 inasema:-
Mkumbukeni BA yule mtu wa Allah wa nchi ya wayunani, mweusi wa sura na umbo la mapambano. Ndipo yule mchungaji mwenye akili na maneno mengi ya kashifa alipoamua kumuingiza siku ya vita kuu ya Bus na wana mpotezaji Loserpool, na alipokwisha kuingia katika mapambano
Demba mwana BA, akawahadaa uyahudi wote na hata yule kijana mzee mtoto wa Gerald alipotaka kukimbia kuokoa hatari iliyomkabili, tayari mpira ulikuwa umeshapita na kufika kwa mwana wa BA ambaye hakutaka kumfadhaisha Mchungaji wake, bila hiyana alitupia mpira nyavuni kupitia kwenye mdoli wa golikipa wa mwana wa wapotezaji.
Mstari wa 3:
Na ikawa kelele yote itokayo Anfilied ikakoma, naam ndipo yule mchungaji alipoweka mabus mawili \ mlangoni mwa kundi lake, na hata ikawa dakika ya mwisho wakishinda vita. Matumaini ya wana wa Brendan yakaishia mstuni, naam na hata sasa ilihali wakiwa huzuni wasipate wa kuwafariji wakabeba watoto wao katika uwanja wao ili kulipoteza lengo la nia yao iliyoleta AIBU katika taifa hilo kwani walipiga kelele sana ili hali mapambano yangali.
Viva viva viva Man City!

0 comments