Liverpool wamekamilisha usajili wa mshambuliaji wa
Ubelgiji Divock Origi kutoka Lille kwa pauni milioni 10.
Origi, 19,
amesaini mkataba wa miaka mitano, lakini atasalia Ufaransa na klabu yake
ya Lille kwa mkopo kwa msimu ujao na atakwenda Anfield msimu wa 2015.
Origi alicheza mechi zote za Ubelgiji katika michuano ya Kombe la Dunia
2014 na alifunga bao pekee katika mchezo dhidi ya Urusi. Alianza kucheza
soka katika klabu ya Genk kabla ya kuhamia Lille akiwa na miaka 15.
Origi anakuwa mchezaji wa sita kusajiliwa na Liverpool, baada ya
kumchukua Rickie Lambert, Adam Lallana na Dejan Lovren kutoka
Southampton, pamoja na Emre Can kutoka Bayer Leverkusen na Lazar
Markovic kutoka Benfica.
0 comments