Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dokta Jakaya Mrisho Kikwete
amesema hatua ya kuhakiki mpaka wa Tanzania na Burundi baina ya nchi
hizo mbili, imelenga kuwafanya wananchi wanaoishi katika maeneo ya
mipakani kutambua maeneo ya nchi zao ili kuwawezesha kufanya shughuli
zao kwa amani na utulivu.
Rais Kikwete amesema hayo katika
uzinduzi wa awamu ya kwanza ya kazi ya uzinduzi wa mpaka baina ya nchi
hizo mbili, na kisha kufuatiwa na mkutano wa hadhara ambao pia
umehudhuriwa na Rais wa Burundi Pierre Nkurunzinza, katika kijiji cha
Mgikomero wilayani Ngara Mkoani Kagera.
Rais Jakaya Kikwete
pamoja na rais wa nchi jirani ya Burundi Pierre Nkurunziza, wamezindua
awamu ya kwanza ya kazi ya utambuzi wa mpaka wa Tanzania na Burundi,
iliyoainishwa upya baada ya mpaka wa kwanza uliochorwa na wakoloni wa
Kiiingereza na Kibelgiji mnamo mwaka 1924.
Katika Mkutano wa
hadhara, Rais Kikwete licha ya kuwataka wananchi wa pande mbili za
Tanzania na Burundi kulinda mpaka huo, amesema serikali yake itaendelea
na kazi ya kuainisha mipaka yake ili kuhakikisha wananchi wa maeneo ya
mipakani wanafanya shughuli zao kwa amani na utulivu.
Kwa
upande wake Rais wa Burundi Pierre Nkurunzinza ameipongeza serikali ya
Tanzania kwa kuendeleza ushirikiano baina ya nchi hizo na kuahidi
kuendeleza umoja na mshikamano baina ya wananchi wake.
Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Profesa ANNA TIBAIJUKA pamoja na
mwenzake wa Burundi Jean Claude Nduwayo wameelezea kiini cha nchi hizo
kuamua kuainisha mipaka yake.
Baadhi ya Wataalam na wananchi wameelezea changamoto walizokumbana nazo kabla ya zoezi hilo.
Jumla ya kilometa mia nne na hamsini zimetumika kuainisha mpaka kati ya
Tanzania na Burundi huku ukigharimu serikali za nchi hizo, zaidi ya
shilingi bilioni mbili nukta sita.
0 comments