Monday, 11 March 2013

AMIA DIGITALI KUTOKA KWA MKANDAMIZAJI

Hii nimekutana nayo katika ukuta wa ukurasa wa mchekeshaji MASANJA MKANDAMIZAJI ndani ya facebook:

"Juzi wakati naelekea Mlimani city nikamkuta mzee mmoja analia pale Mwenge anagalagala kama mtoto huku akilalama haiwezekani haiwezekani serikali gani hii haina huruma na watu wake.

Mwaka juzi wamewahamisha watu wa Kipawa wakawapeleka Chanika, mwaka jana wamewapeleka wengine Mabwepande.

Tena bila msaada wowote ule sasa mwaka huu wanataka watuhamishie digitali! Haki ya Mungu naapa sitoki hapa hata walete greda! Akaniuliza eti mwanangu digitali iko wapi hapa Dar es salaam."
mwisho wa nukuu


--
MSUNI COMPUTER SOLUTION
TUNATATUA TATIZO LA COMPUTER YAKO
065 718 4421
065 714 8283 (habib)
www.aboodmsuni21.blogspot.com

0 comments