Sunday, 10 March 2013

NENO LA SIKU: SIFA

Kila binadamu anapenda kusifiwa na sifa zilizonjema na wengine kufikia hatua ya kutaka kununua sifa njema kwa uongo, kupitia kuhadithi mamba ambayo hayakufanya.

Kujipamba na sifa njema ndio kujijengea heshima katika jamii, na pale unapo jipamba na sifa mbaya hushusha heshima yako katika jamii na mda mwingine kuwa tishio katika jamii na kupelekea jamii kukutenga.

Katika ulimwengu huu wa digitali baadhi ya sifa mbaya zimekuwa ni njema kwa wengi wetu kupelekea kuto ona aibu kujinasibu nazo kama uzinzi (zinaa), kuvaa nguo zi sizo stiri, ulevi, uongo, ukatili na mengineo.

Katika kujipamba na sifa njema lazima kuendane sambamba na kutafuta radhi za Mungu aliyekuumba.

SIFA NJEMA UJENGA HESHIMA, NA UWEZI KUNUNUA SIFA NJEMA


--
MSUNI COMPUTER SOLUTION
NDIO SULUHISHO LA TATIZO YA COMPUTER YAKO
+255-657-148-283 (Habib)
+255-657-184-421 (Msuni)
www.aboodmsuni21.blogspot.com

0 comments