Muhadhara huo utafanyika katika ukumbi wa DYCC uliopo Kariakoo jijini Dar es salaam kuanzia saa mbili na nusu asubuhi siku ya jumamosi ya machi 16 mwaka huo.
Akizungumza na TEMBEZI ZA MSUNI hii leo jioni mratibu wa muhadhara huo Khadija Ibrahim alisema kuwa muhadhara huo utakuwa na wahadhiri mbalimbali ambao ni wasomi wakina mama wa kiislamu wenye taaluma mbalimbali.
Alisema kuwa moja ya mada itakayozungumziwa ni umuhimu wa elimu kwa wanawake wa kiislamu, vile vile watatoa ushauri wa nini shakufanya kutokana na matokeo aliyoyapata katika mitihani yake.
Khadija alihitimisha kwa kusema wanaomba wanadada wote pamoja na mama zao kuhudhuria muhadhara huo kwa kupata mwangaza wa nini cha kufanya.
Muhadhara huo utakuwa wa pili baada wa ule wa awali uliofanyika february 23 mwaka huu, lakini mahudhurio yalikuwa madogo na kutokana na umuhimu wake waandaaji waliamua kupanga siku nyingine ambayo ni machi 16 mwaka huu.
Mnaobwa mufikishiane taarifa pale unapoipata.
--
MSUNI COMPUTER SOLUTION
TUNATATUA TATIZO LA COMPUTER YAKO
065 718 4421
065 714 8283 (habib)
www.aboodmsuni21.blogspot.com
0 comments