Monday, 11 March 2013

NENO LA SIKU: DUA

Dua ni miongoni mwa maneno maarufu midomoni mwa waswhili na limekuwa wimbo kwa timu za Tanzania pale wanapoenda kuiwakilisha nchi.

Kwa haraka haraka dua ni maombezi juu ya kitu fulani kutoka kwa Mungu muumba wa mbingu na ardhi. Kwa namna nyingine dua unaweza ukaitafsiri ni kutaka msaada toka kwa Mungu.

Kuna dua za aina nyingi, kuna za kuomba kinga, za kuomba ufafanuzi juu ya jambo fulani (msaada katika maamuzi), kuomba baraka na kheri, kuomba tiba na nyinginezo.

Kwa upande wa waislam wamefundishwa na mtume (s.a.w) dua za namna mbalimbali, kuanzia anapo amka, anapo kwenda chooni, anapo kula, anapo toka nyumbani kwake, anapo kutana na nduguyake, anapo katiza eneo la makaburi na sokoni, anapoingia nyumbani kwake, na mpaka anakuja kulala.

Mungu ndie anaetufahamu vizuri na lazima tuhitaji msaada toka kwake, kama unavyohitaji 'menu book' ya mashine uliyoinunua ma moja ya njia ya kuomba msaada ni dua.

Ewe ndugu yangu na kusihi usilale usiku wa leo na siku nyingine bila kutanguliza dua. na kila unalo lifanya tanguliza jina la Mungu.


--
MSUNI COMPUTER SOLUTION
NDIO SULUHISHO LA TATIZO YA COMPUTER YAKO
+255-657-148-283 (Habib)
+255-657-184-421 (Msuni)
www.aboodmsuni21.blogspot.com

0 comments