Hekima ni neno maarufu mdomoni mwetu ambapo kila mtu anaweza kulitafsiri ajuavyo, wengi wetu tunaegemea kwenye busara tukija kulitafsiri neno hilo ambalo linaweza likaenda mbali zaidi.
Kwa mujibu wa mukhutubiaji wa leo hekima ni kuwa jambo mahala pake panapostahili ambapo ni vigumu kuleta mtafaruku huko baada ama madhara, akitolea mifano ya matukio aliyoamuru mtume (s.a.w).
Katika moja ya darsa ya mtume (s.a.w) ndani ya msikiti aliingia bedui mmoja na kujisaidia kwenye moja ya kona ya msikiti, kitendo kilichotaka kuwapelekea maswahaba kwenda kumkatiza haja yake lakini mtume (s.a.w) aliwazuia maswahaba zake na pale alipo maliza haja yake aliamuru kumwagiwe maji.
Huo ni mfano mmoja wapo wa hekima kutoka kwa mtume (s.a.w) mfano mwingine unapatikana kwa nabii Sulayman na ndege wake wa hudhud pale alipokosekana katika muhadhara wa jeshi lake na Sulayman (a.s) kuwa nadhiri ya mambo mawili atakapo rejea moja ni kumuadhibu na jingine kumsamehe kama atakuja na sababu zinazoeleweka.
Ewe ndugu yangu fanya maamuzi yako kwa kutumia hekima.
--
MSUNI COMPUTER SOLUTION
NDIO SULUHISHO LA TATIZO YA COMPUTER YAKO
+255-657-148-283 (Habib)
+255-657-184-421 (Msuni)
www.aboodmsuni21.blogspot.com
0 comments