Friday, 8 March 2013

WAISLAM KUFANYA ITIQAF KESHO KUOMBA KINGA, MASHEKHE KUKUTANA KUJADIRI MUSTAKABALI WA NCHI

Waumini wa dini ya kiislamu wanataraji kufamya maombezi maalum ya kuomba kinga kutoka kwa Allah (s.w) hapo kesho jumamos katika msikiti wa kichangani uliopo Magomeni jijini Dar es salaam.

Aliyetoa khutuba ya swala ya ijumaa katika msikiti wa Mtambani, akizungumza baada ya swala ya ijumaa na dua ya kuwaombea udhalilishaji wale wote wanaofanya ukatili, alisema katika itiqafu ya kuiombea kinga kutoka kwa Allah (s.w) itahudhuriwa na mashekhe mbalimbali akiwemo Shekhe Nurdin Kishki.

Maombezi hayo yatakayo anza baada ya swala ya insha katika msikiti wa kichangani itakuwa ni ya kuomba wasifikwe na madhira ama adhabu toka kwa Allah (s.w) inayosababishwa na hali ilivyo ndani ya Tanzania kwa sasa.

Mtoa khutuba katika khutuba yake alisema kuwa moja ya sababu inayopelekea Somalia kuto tawalika mpaka sasa ni kutokana na kunjinjwa hadharani wanazuoni wa kiislam 30 ndani ya Somalia na kupelekea Allah (s.w) kuwashushia ghalika ya kukosa amani.

Mughutubiaji aliwataka waislam wajiokeze kwa wingi katika itiqaf hiyo itakayo fanyika hapo kesho baada ya swala ya insha.


Katika hatua nyingine mashekhe toka kona mbalimbalh za nchi ya Tanzania wanataraji kukutana mwishoni mwajuma hili katika hoteli ya Lamada, jijini Dar es salaam kuzungumzia mustakabali wa nchi ya Tanzania.


--
MSUNI COMPUTER SOLUTION
TUNATATUA TATIZO LA COMPUTER YAKO
065 718 4421
065 714 8283 (habib)
www.aboodmsuni21.blogspot.com

0 comments