Ni kawaida mtu kusifiwa baada ya kufa ama baada ya kuachia wadhifa katika taasisi ama kampuni kwa utendaji wake mzuri. Nilikuwa najiuliza, kwanini huwa ni ngumu mtu kusifiwa wakati bado yuko hai ama akiwa katika nyadhifa anayohodhi ndani ya taasisi ama kampuni?
Mwishoni mwa mwaka jana raisi aliyemaliza/anayemaliza mda wake Leodger Tenga alitangaza kutokitetea kiti chake cha uraisi katika chaguzi ulipangwa kufanyika february 22 mwaka huu, kabla ya kusogezwa mbele mpaka tarehe mpya itakapo tangazwa.
Baada ya kutoa tamko hilo wadau mbalimbali wa mpira wa miguu walisikika kupitia vyomba vya habari wakimsifu kwa uwamuzi huo mzito ukienda sambamba na uletaji utulivu ndani ya soka la bongo.
Hata mie nilishawishika kutaka kuandika makala ya kumpongeza, ila nika kumbuka mvutano baina ya Tff na klabu ya ligi kuu Africa lyon kutotatuliwa zaidi ya mmiliki Zamunda kutumia busara ya kuyajamazia.
Hakuna anaejuwa sakata la mshambuliaji niliyekuwa namzimia Yusuph Soka lilipo ishi baina ya lyon na TFF, pamoja na lile la mshambuliaji aliyekuwa pacha wa Soka katika harakati ya kusaka tiketi ya kupanda ligi kuu ya vodacom Mbwana Samata.
Hilo la lyon na TFF si sababu ya kushindwa kumsifu Tenga kwa kuweka utulivu katika miaka yake 8 yauongozi, ila kigugumizi changu kiliongezeka pale masuala ya pingamizi yalipo anza na kuishia.
Nikasimamisha kalamu pale Wambura alipo ibua suala la katiba na serikali kuamua kufuatilia kama maneno Wambura yana ukweli ndani yake na kujiridhisha na kauli ya Wambura baada ya uchunguzi yakinifu.
Naamini kwa sasa kila mdau wa soka anajua katiba ya TFF ya mwaka 2012 haikufuata taratibu na kupelekea kuwa batili kitendo ambacho Tenga na TFF hawataki kukubaliana nalo.
Kutokana na ubishi wa Tenga na TFF tunaweza kujikuta tunafungiwa na FIFA, sioni tatizo la Tenga kama alivyosifiwa sana mwanzoni mwa mwaka huu na mwishoni mwa mwaka jana kukubaliana na hali halisi kwa kukubali katiba ni batili.
Hakika Tenga umenipa somo la kutomsifu mtu halikuwa bado yuko madarakani, ila bado ujachelewa kuhifadhi heshima yake aliyoijenga ndani ya miaka 8 ya uongozi wake ndani ya TFF.
--
MSUNI COMPUTER SOLUTION
TUNATATUA TATIZO LA COMPUTER YAKO
065 718 4421
065 714 8283 (habib)
www.aboodmsuni21.blogspot.com
0 comments