Chama cha mpira wa miguu nchini Ghana GFA, kimekanusha taarifa
iliyotolewa na joy fm, kuwa katika kambi ya timu ya taifa hilo (Black
stars) kuna mgomo.
Kwa mujibu wa Joy FM "mgomo wa wachezaji ulilazimisha Ghana kufuta
mkutano na waandishi wa habari siku ya jumanne (jana)".
GFA imesema "tunasisitiza kuwa taarifa hiyo si ya kweli na haina msingi."
Black stars inayonolewa na Kwesi Appiah ipo nchini Brazili kushiriki
michuano ya kombe la dunia ambapo ilipoteza mchezo wa awali siku ya
jumatatu mbele ya Marekani na sasa wanajianda kuwakabili Ujerumani.
0 comments