Mtandao wa klabu ya barcelona leo (jumatano) umeripoti kuwa klabu
hiyo inatarajia kuingia mkataba wa miaka 4 na nahodha wa timu ya taifa
ya Chile Claudio Bravo kutaka katika klabu ya real sociedad.
Bravo mwenye miaka 31 anatarajiwa kujiunga na barcelona mara baada ya
kwisha kwa michuano ya kombe la dunia inayoendelea nchini Brazil,
ambapo anatazamiwa kuwa mrithi wa kipa raia wa Hispania Victor Valdes
aliyemaliza mkataba wake wa kuitumikia Barcelona.
Kipa huyo wa Chile aliyoiongoza timu yake kutinga hatua ya 16 bora
mbele ya Hispania na Austaria, ameitumikia Real sociedad.
Katika taarifa iliyowekwa kwenye mtandao wa Barcelona haijaeleza
halama ya usajili wa nahodha huyo wa Chile ambaye anatarajiwa kuungana
na Mchile mwenzake Sanchez katika klabu ya Barcelona.
0 comments