Mume mwimba injili Flora Mbasha, Emanuel Mbasha jana alipandisha
kizimbani na kusomewa mashtaka mawili ya ubakaji ambayo aliyakana
katika mahakama ya Ilala jijini Dar es salaam.
Wakili wa serikali Nassoro Katuga akisoma mashtaka ya Mbasha mbele ya
hakimu Wilberforce Luhwango, alisema mshatakiwa anadaiwa kumbaka
shemeji yake na mfanyakazi wake.
Mei 23 katika eneo la Tabata kimanga mshtakiwa alimbaka shemeji yake
na mei 25 alimbaka mfanyakazi wake katika eneo la Tabata kimanga
jijini Dar es salaam.
Mshitakiwa alikana mashtaka yote mawili na kurejeshwa rumande kwa
kushindwa kufikia masharti ya dhamana ambayo ni kuleta wadhamini
wawili kutoka taasisi za serikali wasaini kulipa shiling milioni tano.
Mashataka yake yatasomwa tena mnamo juni 19 mwaka huu.



0 comments