Monday 30 March 2015

WACHEZAJI 15 WALIMWA KADI NYEKUNDU KWA PAMOJA NDANI YA MCHEZO MMOJA


Wachezaji 15 walionyeshwa kadi nyekundu baada ya kutupiana makonde katika mechi ya ligi ndogo nchini Uturuki.

Wachezaji 15 waonyeshwa kadi nyekundu baada ya kutupiana makonde katika fujo iliyozuka baada ya mchezaji mmoja kuchezewa visivyo katika dakika za lala salama.

Vurugu na ghasia ilizuka huku wachezaji hao wakikabiliana katika mechi hiyo ya ligi ndogo baina ya Yagcilar na Hamzabeyli katika mkoa wa Manisa nchini Uturuki.

Refa wa mechi hiyo Yasin Saygili aliwaadhibu wachezaji 15; 7 kutoka timu ya Yagcilar na 8 kutoka Hamzabeyli na kupuliza kipenga cha mwisho. 


Chanzo: TRT Swahili

0 comments