Gazeti la ash-Sharq linalochapishwa nchini Qatar limefichua kwamba, madola ya Magharibi yanafanya njama za kuzuia maendeleo katika ulimwengu wa Kiislamu.
Gazeti hilo limeandika kwamba, madola ya Magharibi yameanzisha njama za kuushughulisha ulimwengu wa Kiislamu na mambo yasiyo na maana ili kwa njia hiyo zizuie maendeleo ya nchi za Kiislamu.
Kwa mujibu wa gazeti hilo, Wamagharibi wamekuwa wakifanya njama za kuuonyesha Uislamu kwamba, ni tishio kwa utamaduni na ustaarabu wa Magharibi ili kwa njia hiyo waweze kufikia malengo yao.
Ripoti ya gazeti la ash-Sharq la Qatar inazidi kufichua kwamba, kuna njama na mikakati maalumu imeanzishwa na madola ya Magharibi ya kuhakikisha kwamba, ulimwengu wa Kiislamu unashughulishwa na mambo yasiyo na maana pamoja na mivutano isiyokwisha na hivyo kusahahu kujihusisha na masuala ya kielimu pamoja na kupambana na hali ya kubaki nyuma kimaendeleo.
0 comments