Na Sanga Festo
TANESCO wameshafanya yao(umeme umekatika)!!!Umeme wenyewe umeshapanda bei,gharama(Tsh.elfu 10 unapata Unit 8 tu).Licha ya Gharama kupanda,Mgao ndio kwanza unaonekana kurejea Kwa kasi.Ni maumivu Juu ya Maumivu.
Nadhani tukifanya SENSA ya Haraka tu,Wapangaji wengi wanakorofishana,kununiana,kupangiana vitu vya kutumia umeme kwa kipindi hiki kwa kasi kubwa kuliko miaka yote tokea Tanzania iwe Tanzania.
MNAOSHABIKIA SERIKALI TATU,Hii hali ya Kupanda kwa Bei ya Vitu itakuwa mara mbili(Tutalia na Kusaga meno).
Bajeti ya Serikali hiii tuliyonayo ni yakuungaunga.
Sasa mnataka muongeze ya Tatu,Hiyo serikali ya Tatu Bajeti yake
itapatikana kwa Njia ya Kodi,Hivyp mtegemee Kupanda Gharama za Maisha
maradufu.
Serikali ya Tanganyika na Serikali ya Muungano bajeti zake zitakuwa sawa kutokana na ukubwa wa Territory,Ukubwa
wa Wizara na Ofisi ya Waziri Mkuu.Zanzibar wao Mapato yao kwa mwaka ni
Billion 150 na Matumizi yao Kwa Mwaka yanakwenda Billion 300.
SASA Hao Wazanzibary Watahangaika na Serikali ya Muungano ya nini wakati
mapato yao ndio hayo,Hata sasa kwenye Serikali Mbili Zanzibar
hawachangii chochote kuendesha serikali ya Muungano(Tanganyika ndio kila kitu).
Narudia tena Serikali Tatu ni Mzigo kwa Nchi.TUPINGE VIKALI Wanaoipendekeza(Rejea Warioba alisema TUME INAPENDEKEZA MUUNDO WA SERIKALI TATU) hawajawahi ishi ndani ya serikali hiyo,na hawanachakupoteza na Serikali Tatu zitaleta Mzigo kwetu vijana na sio rika la waliopendekeza.
KAma wewe unaona kwasababu CCM ndio inapendekeza serikali mbili,Basi
kwa Ujinga wako wa kupinga kila kitu cha CCM unapinga na hili bila
kufikiria kuwa Kodi itakapopanda hapa haitakuwa kwa WanaCCM tu ni Kwa
Watanzania wote.
Note:SWALA LA KUVUNJIKA KWA MUUNGANO SI KWA
SABABU YA MFUMO WA SERIKALI,NI DHAMIRA YA WAHAFIDHINA WACHACHE
WANAODHANI ZANZIBAR IKIJITENGA ITABAKI SALAMA,AU ITATAJIRIKA
SANA,WANASAHAU UPEMBA NA UUNGUJA ULIOFICHWA NA HUU MUUNGANO TULIO NAO.
0 comments