Kitabu hicho chenye kichwa kisemacho, 'Wasioonekana - Hadithi za Jamii Fiche nchini Kenya', kimeandikwa na aliyekuwa mwanahabari na mwanaharakati wa kutetea haki za mashoga, Bw Kevin Mwachiro.
Kitabu hicho chenye kurasa 114 kinajumuisha mkusanyiko wa hadithi za watu ambao wanadaiwa kupitia hali ngumu baada ya kudhihirika kuwa ni mabasha katika maeneo yote nchini.
Kulingana na Bw Mwachiro, 40, kuna Wakenya wengi ambao hawajaweka hadharani kuwa wana uhusiano na watu wenye jinsia moja kutokana na hofu ya kutengwa na jamii.
Hafla ya uzinduzi wa kitabu hicho, jijini Nairobi iliyohudhuriwa na wanaharakati mbalimbali wa kueteta haki za mashoga, Bw Mwachiro alisema mashoga wamenyimwa nafasi yao katika jamii nchini Kenya.
“Naamini kitabu hiki kitaifanya jamii kuamini kuwa mashoga wanapatikana katika maeneo yote nchini Kenya na wala sio Mombasa,” akasema Bw Mwachiro ambaye alikuwa mwandishi wa habari wa Shirika la Habari la Uingereza (BBC).
“Kwenye Jarida la kitabu changu kuna mguu wa mtu ambaye huwezi ukatambua ikiwa ni mwanamke au mwanaume, hiyo ina maana kuwa watu unaokutana nao mitaani huwezi hukawatambua kuwa wana uhusiano wa aina gani,” alieleza.
Kenya ni miongoni mataifa ya Kiafirika ambayo yameharamisha ndoa za jinsia moja. Hata hivyo, mashoga wanadai kuwa ushoga na usagaji vimejumuishwa katika katiba kwani katiba imempatia Wakenya haki ya kushirikiana na mtu yeyote.
Barani Afrika, nchi ya Afrika Kusini ndiyo ilikuwa ya kwanza kuhalalisha ndoa za jinsia moja mwaka wa 2006.
Bw Binyavanga ambaye alikuwepo katika uzinduzi huo aliwataka mashoga ambao wanaona haya kujitangaza wafanye hivyo huku bado wakiwa hai.
Bw Binyavanga alipasua mbarika kuwa ni shoga wiki mbili zilizopita jambo ambalo lilileta mjadala mkali nchini huku baadhi wakimtaja kama shujaa ilhali wengine wakishutumu hatua hiyo.
Tukio hili ni muhimu kwa jamii ya kiislamu kuweka tahadhari kwa malezi ya watoto na kutilia mkazo zaidi mafundisho ya dini vinginevyo ni kuandaa kizazi kiovu huko baadae.
![]() |
Nakala za kitabu cha mashoga kilichozinduliwa Nairobi Jumatano |
0 comments