Sheikh Hamid Masoud Jongo ni imamu wa msikiti wa manyema na kundecha ni Mwenyekiti wa Baraza kuu la Jumuiya na Taasisi za Kiislamu nchini ambaye pia ni Amir wa Shura ya Maimamu. Sheikh Hamid Masoud Jongo na Mussa Yusuf Kundecha wameteuliwa kupitia uwakilishi wa taasisi za dini.
Wajumbe wengine waliochaguliwa kuwakilisha taasisi za dini za kiislamu kutoka Tanzania Bara ni Tamrina Manzi, Shamim Khan na Hamisi Ally Togwa. Kutoka upande wa Tanzania Zanzibar ni Sheikh Thabit Nouman Jongo, Sheikh Nassoro Mohammed Ibrahimu, Fatma Mohammed Hassan, Yasmin Yusufali E. H alloo na Thuwein Issa Thuwein.
Bunge hilo maalum linaundwa na Wajumbe 635 ambao 358 ni kutoka bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Wajumbe 76 kutoka Baraza la Wawakilishi Zanzibar na Wajumbe 201 kutoka mashirika yasiyo ya kiserikali na taasisi za dini.
Sheikh Mussa Kundecha |
Sheikh Hamid jongo |
Sheikh Thabit Nouman Jongo, naibu katibu wa Mufti Zanzibar |
Shamim Khan, mwenyekiti taifa wa baraza la wanawwake-Bakwata |
0 comments