MGANGA wa kienyeji, Yahaya Michael (34) amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Ilala kujibu mashitaka ya wizi wa gari.
Mwendesha Mashitaka wa Serikali Ester Kyala alidai mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Hassani Juma, Januari 20 mwaka huu, eneo la mtaa wa Mafia Kariakoo Wilaya ya Ilala, Michael aliiba gari lenye namba za usajili 139 BSJ aina ya Toyota Rav 4 mali ya Ederick Elieza.
Mshitakiwa alikana mashitaka na alirudishwa rumande baada ya Wakili wake Tausi Kheri kuiambia Mahakama kuwa wadhamini wa mshitakiwa hawajafika.
Hakimu Juma alimtaka kuwa na wadhamini wawili wa kuaminiwa watakaosaini kulipa Sh milioni sita na kuzipeleka mahakamani hapo. Kesi itatajwa Machi 17 mwaka huu.
Wakati huohuo, watu watano wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Ilala kujibu mashitaka ya kukutwa na dawa za kulevya aina ya heroine.
Watu hao ni Yassin Seleman (25), Ally Kisoba (28), Hemed Idd (28), Frank Thomas (26) na Adam Mohammed (37). Wote wakazi wa Kiwalani.
Kyala alidai mbele ya Hakimu Juma kuwa Februari 21 mwaka huu, eneo la Kiwalani Kigilagila Wilaya ya Ilala, walikutwa na gramu 18 za heroine zenye thamani ya Sh 38,000 kinyume na sheria.
Washitakiwa walikana mashitaka na wamerudishwa rumande kwa kukosa wadhamini.
Kesi itatajwa Machi 17 mwaka huu. Hakimu Juma aliwataka kuwa na wadhamini wawili kila mmoja ambao watasaini kulipa Sh 20,000.

0 comments