RAIS Jakaya Kikwete, amemtumia Salamu za Rambirambi Mufti wa Tanzania, Sheikh Shaaban Bin Simba, kutokana na msiba wa Shekhe wa Mkoa wa Iringa, Alhaj Shekhe Ally Juma Tagalile (96). Shekhe Tagalile alifariki usiku wa kuamkia leo katika Hospitali ya Mkoa wa Iringa, alikokuwa amelazwa akisumbuliwa na ugonjwa wa shinikizo la damu.
“Nimeshtushwa, nimesikitishwa na kuhuzunishwa na taarifa za kifo cha Shekhe wa Mkoa wa Iringa, Alhaj Shekeh Ally Juma Tagalile, kilichotokea usiku wa kuamkia jana,” amesema Rais Kikwete katika salamu zake zilizotumwa na Kurugenzi ya Ikulu Mawasiliano.
Rais Kikwete amesema kifo cha Shekhe Tagalile ni pigo siyo tu kwa waumini wa dini ya Kiislamu mkoani Iringa, ambao hakika walikuwa wanamtegemea katika uongozi na katika masuala ya kiroho, bali pia kwa waumini wa dini hiyo kote nchini.
“Natambua kuwa enzi za uhai wake, Shekhe Tagalile pia alitoa mchango mkubwa katika Utumishi wa Umma hususan katika Sekta ya Afya akiwa na Taaluma ya Udaktari, hivyo kuondoka kwake kumetunyang’anya kama Taifa uzoefu wake mkubwa katika taaluma ya afya,” alisema Rais Kikwete katika kuomboleza kifo chake.
“Kutokana na msiba huo mkubwa, ninakutumia wewe Mufti wa Tanzania, Shekhe Shaaban Bin Simba, salamu zangu za rambirambi na pole nyingi kwa kumpoteza mmoja wa viongozi wa ngazi ya juu wa dini ya Kiislamu hapa nchini.
“Ninamuomba Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, aipokee na kuilaza Mahala Pema Peponi Roho ya Marehemu, Shekhe Tagalile, amina,” alieleza Rais Kikwete katika kuomboleza msiba huo.
Rais Kikwete amemuomba Mufti Simba kumfikishia salamu zake za rambirambi na pole nyingi kwa familia ya marehemu kwa kupotelewa na kiongozi na mhimili muhimu wa familia.
Amewaomba wawe na moyo wa uvumilivu na ujasiri, ili wahimili machungu ya kuondokewa na mpendwa wao kwa kutambua kuwa yote ni mapenzi yake Mola.
Aidha Rais Kikwete ameihakikishia familia ya marehemu kuwa yuko pamoja nao katika kipindi chote cha kuomboleza kifo cha mpendwa wao kwani msiba huu ni wa wote.
CHANZO: HABARI LEO

0 comments