Kama ilivyokuwa imetarajiwa na wengi mwigizaji
mashuhuri kutoka Kenya Lupita Nyong'o amenyakuwa tuzo la Oscar la
mwigizaji msaidizi wa kike kwa jukumu lake la kuelezea masaibu ya Patseh
katika filamu ya utumwa ya ''12 Years A Slave.''
Kisha Lupita akaongeza kusema, " Na iwe ukumbusho kwangu na kila mtoto kwamba kokote unakotoka, ndoto zako ni halisi.''
Mwigizaji Jared Leto alinyakuwa tuzo la mwigizaji bora msaidizi wa kiume kwa jukumu lake la kuelezea maisha ya mwanamke aliye na jinsia mbili aliyekuwa na akiishi na virusi vya HIV katika filamu Dallas Buyers Club.
Alilazimika kupunguza uzani kwa kipindi kifupi ili kuigiza. Sherehe ya kutolewa kwa tuzo hizo zimefanyika mjini Los Angeles nchini Marekani.
chanzo: bbc swahili
0 comments