Monday, 3 March 2014

MADAKTARI WASIO NA MIPAKA WAZUIWA KUKUTANA NA WAISLAMU WA MYANMAR, WARUHUSIWA MIJI MINGINE

By    

 https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiAJlapjgc_WlrBxwHi1bv_GkhtowRBf5BreAvKHnSDE6q0joHGhs9wcRyc9ZxjYD8dPdzZi2E5oDDRjRiNvyd-4TB9TfKd5LxBGEFMI3MsnLNrLaRpK3KWcNAY_WEuOBg3ilmgj2r_K8yl/s280/Burma-HIV-patient-011.jpg

Serikali ya Myanmar imewakataza  Shirika la Madaktari Wasio na Mipaka (MSF) kuingia katika jimbo la Rokhine wanaloishi  Waislamu  wengi kwa shabaha ya kuwapatia matibabu. 

Taarifa iliyotolewa na madaktari hao imeeleza kuwa, hali ya kimaisha inayowakabili Waislamu katika jimbo hilo ni ya kutisha na kusikitisha, kwani watu hao wanahitaji misaada ya kibinadamu haraka iwezekanavyo. 

Serikali ya Myanmar imekataa kutoa ruhusa kwa madaktari wasio na mipaka kulitembelea jimbo la Rokhine kutokana na kukasirishwa na ripoti iliyotolewa na madaktari hao mwezi Januari kuhusiana na ukatili unaofanywa na Mabudha wa kuauwa kwa halaiki Waislamu  nchini humo. 

Aidha serikali hiyo imetoa ruhusa kwa madaktari hao kutembelea miji ya Kashin na Shan. Hata hivyo serikali ya Myanmar haijatoa taarifa rasmi kwa nini imewazuia madaktari hao kuingia jimbo la Rokhiene ambako kunahitajika mno msaada wa kidaktari.

Tokea mwaka 2012 Waislamu wa Myanmar wamekuwa wakivamiwa na kushambuliwa, kuuawa na kuchomewa moto nyumba zao, bila ya serikali ya nchi hiyo kuchukua hatua zozote. 

Mashirika ya kutetea haki za binadamu yaliripoti hivi karibuni vitendo vya kinyama vinavyofanywa na askari usalama wa Myanmar vya kuwateka nyara wanawake na mabanati wa Kiislamu wa kabila la Rohingya, kuwapiga, kuwalazimisha kutumia dawa za kulevya na kisha kuwanajisi katika kambi za kijeshi.

Hata hivyo Serikali ya Myanmar imerejea kukataa ripoti za MSF, Umoja wa mataifa na makundi ya haki za binadamu.


chanzo: ahbaabul rasul

0 comments