Saturday, 1 March 2014

SHUNGI RUKSSA KATIKA MCHEZO WA MPIRA WA MIGUU

By    
Image
Shirikisho la soka la dunia "FIFA" wameruhusu ufaaji wa shungi ama kofi wakati wa kushiriki mchezo wa mpira wa miguu.

Ruhusa hiyo itawaruhusu mabinti wa dini ya kiislamu na dini nyinginezo zinazo kataza mwanamke kuonyesha kichwa chake hadharani, kushiriki katika mchezo huo wa mpira wa miguuu huku wakiendela kuwa katika hifadhi ya kichwa chao.

"Ilikuwa imeamuliwa wachezaji wa kike kufunika kichwa wakati wa mchezo," alisema Jerome Valcke ambaye ni general secretari wa FIFA. wakati wa mkutano wa vyama vya kimataifa vya mpira wa miguu (IFAB) uliofanyika Zurich.

"Na pia wachezaji wa kiume nao wanaruhusiwa kucheza wakati vichwa vyao vimefunikwa," alisema Valcke. Japokuwa havitakuwa sawa na wanavyo vivaa kila siku.

Aliongeza kuwa kipachiko hicho cha kichwani kinatakiwa kiendani na rangi za jezi za timu husika.

0 comments