Idara ya polisi mjini New York Marekani, imefunga
kitengo chake maalum cha ujasusi ambacho huwapepeleza waisilamu ili
kuchunguza kama kuna tisho lolote la ugaidi.
Vyombo vya habari nchini Marekani vinasema kuwa kitengo hicho kiliwahi kushitakiwa mara mbili kwa mbinu zao za ujasusi na pia kulaaniwa na makundi ya wanaharakati wa haki za binadamu.
Pia kiliwaghadhabisha waisilamu hasa kwa kuwachunguza.
"mageuzi haya ni hatua muhimu sana katika kuondoa hali ya wasiwasi na kutoaminiana kati ya polisi na jamii ili jamii iweze kusaidia polisi kuwashika wahalifu,'' ilisema taarifa kutoka katika ofisi ya meya wa New York Bill de Blasio.
'Vita vya kisaikolojia'
Hatua ya kusitisha mpango huo, ilifikiwa na kamishna mpya wa polisi wa kituo hicho, na inaonekana kama njia moja ya kubadili mbinu za kukusanya ujasusi ambazo wengi wanasema zilichangia mashambulizi ya Septemba 9/11
Kitengo hicho, kilichoanzishwa mwaka 2003, na baadaye kuitwa, ' Zone Assessment Unit ' kilipeleleza waisilamu hasa maeneo walikofanya kazi, kuswali, kununua madukani na hata mikahwa walikokuwa wanakulia.
Wakuu wa kitengo hicho wanasema kuwa kazi yao iliathiri sana uhusiano kati ya jamii na polisi
0 comments