Winga Real Madrid Angel Di Maria (27), huenda akakataa kuijiunga na Manchester United licha ya kutengewa mshahara wa 150,000 kwa wiki imeripotiwa na Daily Express.
Daily Express imeripoti pia Chelsea huenda ikamchukuwa Javier Pastore kutoka PSG kwa pauni milioni 25 iwapo mabingwa hao wa Ufaransa watamchukua Angel Di Maria anae waniwa pia na Manchester united.
Na Sunday Times imeripoti Angel Di Maria angependa kwenda Paris Saint-Germain badala ya Manchester United ambayo haichezi Champions League msimu ujao.
KUTOKA SUNDAY TELEGRAPH
- Juventus wanajipanga kutoa pauni milioni 20 kumchukua Paulinho (25) kutoka Tottenham, hatua hiyo huenda ikatoa mwanya kwa Manchester United kumchukua Arturo Vidal (27)
- Van Gaal (62) amemwambia winga Arjen Robben kuwa anakaribishwa Old Trafford.
KUTOKA THE SUN ON SUNDAY
- Mshambuliaji wa Ecuador Enner Valencia, 25, amewasili London kukamilisha uhamisho wake kwenda West Ham kutoka klabu ya Pachuca ya Mexico.
- Dynamo Moscow wanataka kumchukua Wilfired Zaha, 21, kutoka Manchester United baada ya kumchukua Alex Buttner.
KUTOKA MAIL ON SUNDAY
- Manchester City wanakaribia kumsajili beki wa kati wa Ufaransa Eliaquim Mangala, ambaye Manuel Pellegrini anaamini atacheza vyema na Vincent Kompany.
KUTOKA SUNDAY EXPRESS
- Boss mpya wa Manchester United Louis van Gaal, ambaye huenda akaingia rasmi Old Trafford siku ya Alhamisi, anatarajia kuwasajili Mats Hummels na Marco Reus.
KUTOKA Caughtoffside.com
- Liverpool wanajiandaa kutoa pauni milioni 26 kumsajili Romelu Lukaku, 21, kutoka Chelsea.
KUTOKA SUNDAY MIRROR
- Newcastle imewasiliana na Monaco kujaribu kumsajili mshambuliaji Emmanuel Reviere, 24.
KUTOKA TALKSPORT
- AC Milan wamesema hawatomsajili tena beki Sime Vrsaljiko ambaye anasakwa na Arsenal.
KUTOKA DELLO SPORT
- Beki wa kati wa Roma Mehdi Benatia anataka kuhamia Chelsea.
KUTOKA MUNDO DEPORTIVO
- Barcelona wanamtazama kwa karibu beki wa Tottenham Jan Vertonghen. Barca pia wanamfuatilia Mats Hummels wa Borussia Dortmund.
KUTOKA A BOLA
- Mshambuliaji wa Manchester United Bebe amefikia makubaliano na Benfica ya uhamisho wa kudumu. Klabu hizo mbili bado hazijakubaliana bado kuhusu ada.
KUTOKA SUNDAY PEOPLE
- Licha ya kununua wachezaji watatu mpaka sasa, boss wa Liverpool Brendan Rodgers anataka kununua wachezaji wengine sita. Rodgers ameambiwa anaweza kutumia kitita chote cha kumuuza Luis Siarez, na henda akatumia hadi pauni milioni 135.
- Luis Suarez huenda akakatwa pauni milioni 3 katika mshahara wake wa pauni milioni 10 kwa mwaka ikiwa atamng'ata mchezaji mwingine akiwa Barcelona.
0 comments