Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Nec, Ramadhani Kailima. |
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Nec, Ramadhani Kailima (pichani), kuahirishwa kwa tarehe ya kuanza uhakiki taarifa za wakazi wa mkoa huo waliojiandikisha katika daftari hilo, utaanza Agosti 18 hadi 22, mwaka huu.
Kailima alisema hatua hiyo inatokana na changamoto za mifumo ya uchakataji wa taarifa za wapigakura ili kuondoa mapungufu yanayoweza kujitokeza na kuchukua muda wa kukamilisha uchapaji wa daftari la awali la wapigakura kwa mkoa huo.
Alisema kutokana na changamoto hizo, tume inawatangazia wakazi wa mkoa huo kuwa daftari hilo litawekwa wazi kwa ajili ya kukaguliwa kuanzia kesho hadi Jumamosi ijayo.
“Tunawaomba wananchi wote wajitokeze kukagua daftari hilo kwa tarehe litakapowekwa wazi katika ofisi za kata au manispaa za Ilala, Temeke na Kinondoni au kwa kutumia namba *152*00# kisha wafuate maelekezo, ili kama kuna mapungufu yaweze kufanyiwa kazi kabla ya kuchapa daftari la mwisho litakalotumika siku ya mwisho,” alisisitiza Kailima katika taarifa yake kwa vyombo vya habari jana.
Wiki iliyopita Nec ilitangaza kuanza kuhakiki kwa taarifa za wapiga kura kwa mkoa huo Agosti 15 hadi 19, mwaka huu.
CHANZO: NIPASHE
0 comments