Mbunge wa jimbo la mafinga mjini Cosato Chumi akiwasikiliza wafanyabiasha wadogowadogo
NA FREDY MGUNDA,MAFINGA
Mvutano mkali kati ya wafanyabiashara wadogo wadogo (
machinga) mjini mafinga mkoani Iringa na uongozi wa halimashauri
hiyo umeendelea kufukuta baada ya wafanyabiashara hao kugomea kuondoka katika
eneo hilo wakidai maslai ya watu wachache ndio yanayowahamisha katika eneo hilo
jambo lilopelekea mbunge kuingilia kati .
Wakitoa kilio chao mbele ya mbunge wa mafinga mjini Cosato Chumi
wafanyabiashara hao walisema kuwa wamekuwa wakinyanyaswa kwa muda mrefu na
halimashauri hiyo kwa kuhamishwa hamishwa kila kuikicha na kupelekwa
maeneo ambayo siyo rafiki kwa biashara zao .
Mwenyekiti wa wafanyabiashara hao Glibet amoni alisema
hapo awali walikuwa wakifanyia biashara zao bembeni ya soko la mafinga Uwanja
wa mashuja ) na badaye kuja kuhamishwa katika eneo hilo na kupelekwa katika
eneo la Kinyanambo ambalo pia halifai kwa biashara kwa kuwa kipindi cha mvua
vitu vyao huzama kwenye maji kwa kuwa eneo hilo huwa linasimamisha maji pindi
mvua inyeshapo .
Alisema kuwa baada ya kuona eneo hilo linaharibu biashara zao
waliamua kurudi katika eneo lao la awali la mashuja na kuutaarifu uongozi wa
halimashauri hiyo kuwa wamerejea katika eneo hilo lakini walifanya
biashara kwa majuma mawili na baadaye kuja kutangaziwa kuondoka katika eneo
hilo na kwenda katika soko jipya ambalo pia miundombinu yake haijakamilika na
wali sio eneo la wamachinga
Alisema kuwa walishanga kusikia matangazo ya barabarani kuwa
hakutakuwa na mnada katika eneo hilo siku ya jumapili na walipoenda siku hiyo
walikuta magari ya polisi yakiwa yametanda katika eneo hilo kuwazuiya kufanya
biashara katika eneo hili jambo lilizodii kuwadhofisha kwa kuwa wengi wao
nawamikopo katika maeneo mbalimbali na wanapaswa kurejesha mikopo hiyo
“Mh mbunge wewe ndio msaada wetu uliahidi kututetea sana tunaona
kuna mambo ya siasa yanaingia hapa kwani huyu mwenyekiti wa halimashauri
Charles Makoga anatulazimisha kwenda kule kwa kuwa yeye anavibanda vyake kule
sokoni ndio mana analazimisha tupelekwe kule na tushanga kuja
kututangazia kibabe na kuondolewa a na polisi kama vile ni majambazi wakati
ushuru wao tunalipa na eneo huwa tunafanya usafi kwani wanatufanyia hivii au
sisi sio watanzania ”
Waaliongeza kuwa wao siku yao ya kufanya biashara ni siku moja
tu ya wiki yani jumapili lakini wameshanga kuona ungozi wa halimashauri hiyo
kwa kushirikiana na wafanyabiashara wachache wa soko kuu wanaolalamika kutokuza
biadha zao pindi mnada huo unapofanyika katika eneo jambo ambalo siyo la kweli.
Akipokea kilio chao mbunge huyo wa mafinga mji Cosato chumi
awaliwata wafanyabiashara hao kuwa wavumilivu ili kuweza kwenda kuzungumza na
uongozi wa halimashauri hiyo ili kuona ni sababu gani zilizopelekea wao
kutolewa katika eneo hilo na kupelekwa soko jipya eneo ambalo limetegwa kwa
ajili ya soko na wala sio kwa ajili yam nada wa siku moja .
Chumi alisema yeye kama mbunge Hata kubali kuona wananchi wake
wananyanyaswa na watu wachache kwani yeye ni mbunge wa watu wote na wala
hatakubali kuona watu wake wakipelekwa katika maeneo ambayo siyo rafiki kwa
biashara
‘’Kilio chenu nimekisikia na mimi nataka kukimbizana na kasi ya
magufuli ya kuwatetea wanyonge sioni sababu za msingi za nyie kuhamishiwa kule
soko jipya wakati nyie huwa munafanya mnada siku moja tu hao wanaosema hawauzi
kwanini wanakuwa wabinafsi hivyo ase yani wao wanauza siku sita nyie mnada wenu
ni siku moja halafu eti wanasemna hawauzi mi niwambie waache ubinafsi
na hili sitakubaliana nao ’’
Chumi alisema kuwa kimhesabu kupeleka mnada katika eneo hilo
lililojengwa kwa kwa ajili ya soko ni kupoteza mapato ya halimashauri kwani
badala ya kukusanya ushuru wa siku saba kwa wiki watakuwa wanakusanya ushuru wa
mnada ambao ni siku moja kwa wiki jambo ambalo kimahesabu halikubaliki
Kwa upande wake katibu wa ccm wilaya ya Mufindi Jimsoni mhagama
alisema inapaswa busara kutumika katika kuwasimamia wafanyabiashara hao na
kuchana na kutumia ubabe kwani nao wanahaki ya kufanyabiashara kama
wanavyofanya watu wengine .
Mhagama alisema kuwa serekali ya Raisi Magufuli ni serekali
inayowangalia wafanyabiashara wadogo kwa jicho la pili ili waweze kufanikiwa
katika biashara hao na kuwanyanyasa au kuwahamisha bila ya kukaa chini na
kukubaliaba siyo jambo la busra na ofisi yake atajaribu kuangallia jinsi gani
ya kuwasaidia ili wafikie muafaka
0 comments