Dar es Salaam, Februari 17, 2016 - Fastjet
imepunguza mtiririko wa safari zake
kwenye njia ya Kilimanjaro Tanzania na Nairobi Kenya kuanzia Jumatatu
Februari 15, 2016.
Fastjet ambao
awali walikuwa wanatoa safari za kila siku kwenye njia hii hivi sasa watakuwa
wanafanya safari kutoka Uwanja Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta hadi
Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro mara mbili kwa wiki siku za Ijumaa na Jumapili tu.
Mabadiliko
ya mtiririko wa safari utazifanya ndege
za fastjet kuondoka Nairobi kila Ijumaa na Jumapili saa 5.40 na kutua
Kilimanajaro saa 6.40 na safari ya kurudi ndege itaondoka Kilimanjaro saa 7.10
na kutua Nairobi saa 8.10.
Kupunguzwa kwa
safari hizo kumetokana na kuwepo kwa mahitaji kidogo miongoni mwa wateja
nyakati za wiki kutoka masoko yote mawili ya Kilimanjaro na Nairobi na hivyo
kufanya safari za ndege za kila siku kutokuwa nzuri kibiashara kwenye siku hizo.
Shirika hilo
limesema kuwa lengo lake ni kurejesha safari hizo kwenye njia ya Kilimanjaro
–Nairobi pindi tu wateja wake watakapohitaji.
Safari za kila
siku za kutoka Dar es Salaam na
Kilimanjaro hadi Nairobi zilianza Januari 11, 2016.
Mahitaji ya
abiria kwa safari za ndege kwenye njia kubwa ya kibiashara kati ya majiji ya
Dar es Salaam na Nairobi ambayo kwa
pamoja yana idadi ya watu zaidi ya
milioni nane yamekuwa ni ya kuridhisha na fastjet iko kwenye mawazo kuwa ndege moja ni lazima iongezeke kwenye safari
kati ya majiji haya miwili katika siku za usoni.
Matokeo ya safari
za fastjet kwenda Nairobi kutoka Dar es Salaam yamekuwa ni makubwa ambako
kunaelezwa na ukweli kuwa nauli zinazotolewa na mashirika ya ushindani kati
ya nchi hizo mbili zimeshuka kwa kiwango cha hadi asilimia 40 tangu fastjet
waanze safari zake.
Nauli za fastjet kwa kiwango kikubwa zipo chini kuliko zile zinazotozwa
na mashirika mengine kwa safari za moja
kwa moja kati ya Nairobi/Dar es Salaam
ambapo nauli zinaanzia dola 80 kwa safari moja.
Nauli hizo hazijumuishi
kodi ya serikali ambayo ni dola 49 kuondokea Tanzania na dola 40 kuondokea
Kenya na hivyo fastjet kupendekeza wateja wake kufanya maandalizi mapema ili
kutumia fursa hiyo ya tozo la nauli nafuu.
Hata hivyo
fastjet inasisitiza kuwa kupunguza
safari kwenye njia kati ya Nairobi na Kilimanjaro kunafungua fursa ya kuongeza
uwezo kwenye njia za kikanda zilizopo na hali kadhalika uwezekano wa
kuzindua njia nyingine mpya ya kikanda
katika siku za karibuni.
0 comments