Tuesday, 2 February 2016

MANISPAA YA ILEMELA YAWEKA MSIMAMO WAKE DHIDI YA WAFANYABIASHARA WA HOTEL NA NYUMBA ZA KULALA WAGENI

By    
Mkurugenzi wa Manispaa hiyo John Wanga akitoa ufafanuzi kwa Wanahabari juu ya tozo ya Kodi ya Malazi kwa wafanyabiashara wa hotel na nyumba za kulala wageni.
Wafanyabiashara wa Hotel na Nyumba za Kulala Wageni katika Manispaa ya Ilemela Mkoani Mwanza, Wametakiwa kufanya biashara zao kwa mjibu wa kanuni na sheria za biashara zao ikiwemo kulipa ushuru na kodi mbalimbali kama ilivyoidhinishwa na Serikali.

Kauli hiyo imetolewa hii leo na Mkurugenzi wa Manispaa hiyo John Wanga, katika Kikao cha Viongozi wa Manispaa ya Ilemela na Wafanyabiashara hao, juu ya Ufafanuzi wa Sheria ya Kodi ya Malazi, ambayo imeanza kukusanywa kwenye Hotel pamoja na nyumba zote za kulala wageni.

“Kama una wajibu wa kulipa kodi Majengo, leseni ya biashara, mabango, ushuru wa malazi, ushuru wa huduma na kodi nyingine zote zilizo kisheria, ni vyema ukalipa bila kushurutishwa. Kutokufanya hivyo utatufanya twende kwenye ule mkono mwingine ambao tusingependa sana kuutumia ambao ni kushurutishana”. Amesema Wanga.

Hata hivyo licha ya agizo hilo, Wafanyabiashara katika Manispaa hiyo wameiomba Serikali kuwapunguzia mzigo wa Kodi walionao kwa kuwa hivi sasa wanakabiriwa na mzigo mkubwa wa kodi pamoja na Ushuru jambo ambalo wamesema ni tofauti na ahadi ya kuondoa kero ya kodi mbalimbali aliyoitoa Mhe.Rais John Pombe Magufuli wakati wa Kampeni zake.

“Kodi zimekuwa nyingi sana kwa sisi wafanyabiashara wa Hotel na Guest Houses (nyumba za kulala wageni), kwa mfano kodi ya majengo, leseni ya biashara, ardhi, mabango na nyinginezo. Yaani nyumba moja inakuwa na kodi zaidi ya 11 sasa itafika sehemu tutashindwa kufanya biashara. Sisi tuko tayari kulipa kodi ya majengo, ardhi na leseni hivyo serikali iangalie namna ya kutusaidia”. Alisema Nuru Ramadhan ambae ni mmoja wa wamiliki wa nyumba ya kulala wageni katika Manispaa ya Ilemela na kuungwa mkono na wenzake.

Hawa Waziri ambae ni Mwanasheria wa Manispaa ya Ilemela, amewasihi Wafanyabiashara hao kuwa tayari kulipa kodi zilizopo kisheria, ikiwemo Kodi ya Malazi huku wakiendelea kujenga hoja Serikalini ili Sheria hizo zifanyiwe marekebisho bungeni na hatimae kupunguzwa.

Awali Wafanyabiashara wa Hotel na Nyumba za Kulala Wageni, walikuwa wakilipa Kodi ya Malazi ambayo ni asilimia 20 ya mapato yanayotokana na malipo ya kila mteja, kabla ya kodi hiyo kusitishwa na Serikali ambapo hata hivyo imerejeshwa tena na Wafanyabiashara hao wanatakiwa kulipa kodi ya asilimia 10 ya mapato yanayotokana na mteja badala ya 20 kama ilivyokuwa awali.
Kikao juu ya tozo ya Kodi ya Malazi kwa wafanyabiashara wa hotel na nyumba za kulala wageni kikielendelea
Afisa biashara Manispaa ya Ilemela Mkoani Mwanza akitoa ufafanuzi juu ya tozo ya Kodi ya Malazi kwa wafanyabiashara wa hotel na nyumba za kulala wageni
Hawa Waziri ambae ni Mwanasheria wa Manispaa ya Ilemela Mkoani Mwanza akitoa ufafanuzi kwa wanahabari juu ya tozo ya Kodi ya Malazi kwa wafanyabiashara wa hotel na nyumba za kulala wageni
Cyprian Oyier ambae ni mmoja wa wafanyabiashara wa hotel Manispaa ya Ilemela akiwasilisha hoja zake katika kikao juu ya tozo ya Kodi ya Malazi kwa wafanyabiashara wa hotel na nyumba za kulala wageni
Lemmy Muganyizi Mboyelwa ambae ni mmoja wa wamiliki wa nyumba ya kulala wageni katika Manispaa ya Ilemela akiwasilisha hoja zake katika kikao juu ya tozo ya Kodi ya Malazi kwa wafanyabiashara wa hotel na nyumba za kulala wageni
Nuru Ramadhani ambae ni mmoja wa wamiliki wa nyumba ya kulala wageni katika Manispaa ya Ilemela akiwasilisha hoja zake katika kikao juu ya tozo ya Kodi ya Malazi kwa wafanyabiashara wa hotel na nyumba za kulala wageni
Melikior Fundi Minsa ambae ni mmoja wa wamiliki wa nyumba ya kulala wageni katika Manispaa ya Ilemela akiwasilisha hoja zake katika kikao juu ya tozo ya Kodi ya Malazi kwa wafanyabiashara wa hotel na nyumba za kulala wageni
Wafanyabiashara wa hotel na nyumba za kulala wageni katika Manispaa ya Ilemela wakiwa katika kikao cha ufafanuzi juu ya kuanza kutumika kwa kodi ya Malazi
Wafanyabiashara wa hotel na nyumba za kulala wageni katika Manispaa ya Ilemela wakiwa katika kikao cha ufafanuzi juu ya kuanza kutumika kwa kodi ya Malazi
Kushoto ni Stella Lwakatare ambae ni Afisa Biashara Mkuu katika Manispaa ya Ilemela Mkoani Mwanza akifafanua jambo kwenye kikao cha Wafanyabiashara wa hotel na nyumba za kulala wageni katika Manispaa ya Ilemela juu ya kuanza kutumika kwa kodi ya Malazi.
Katikani ni Mkurugenzi wa Manispaa hiyo John Paul Wanga na Kulia ni Peter Revelian ambae ni Mwekahazina wa Manispaa ya Ilemela.
Watumishi wa idara mbalimbali katika Manispaa ya Ilemela Mkoani Mwanza.
Imeandaliwa na George Binagi-GB Pazzo

0 comments