Sunday, 28 February 2016

UTI- URINARY TRACT INFECTION

Imeandaliwa na: AMINA AHMED ©Afyalishe
UTI ni ugonjwa wa jinsia zote, ila wanawake ndio kundi hatarishi zaidi kutokana na maumbile yao.
Ugonjwa huu unaweza kujirudia hata kuchelewa kupona kulingana na ukubwa wa tatizo!

Ugonjwa huu husababishwa na bakteria.
1.Bakteria hawa mara nyingi hupatikana sehemu ya haja kubwa.
2. Tendo la ndoa
3. Utumiaji wa maji yenye bakteria wengi kusafisha sehemu za siri.
4. Kuvaa nguo za ndani zenye unyevu, au za mpira hivyo kusababisha joyo kali linalowawezesha bakteria hawa kukua.
5. Mawe ya figo, kiharusi, kisukari, ujauzito
6. Kwa wanawake kutumia kemikali kujisafisha sehemu za siri pamoja na mavitu ya kuongeza mnato


DALILI

1. Maumivu wakati wa kukojoa.
2. Kukojoa mara kwa mara au kwa wingi au kidogo kidogo.
3. Maumivu ya mgongo au chini ya kitovu.
4. Mkojo wenye rangi na harufu isiyo ya kawaida.
5. Kuhisi uchovu
6. Homa ya kupanda na kushuka.
Bakteria hawa wanaweza kuathiri hadi figo kama ugonjwa hautatibiwa mapema.

VIPIMO

Nenda kituo cha afya ambapo utatakiwa kutoa sampuli ya mkojo.

TIBA

1. Ugonjwa huu unatibiwa kwa antibiotics na maji mengi sana kama mashambulizi ni makubwa.
Pia unaweza pewa dawa za kupunguza maumivu.
2. Pia waweza kunywa maji mengi kuwezesha bakteria kutolewa kwa njia ya mkojo kama ugonjwa upo hatua za awali.

KINGA

1. Usafi wa sehemu za Siri, hapa hushauriwa kunawa kutoka mbele kwenda nyuma.
2. Kujisaidia pindi huisipo haja ndogo kuzuia kuchubua kuta za kibofu na kuongeza uwezekano wa maambukizi.
3. Kunywa maji mengi
4. Kunywa chai kama una historia ya kujirudia huu ugonjwa
5. Kusafisha sehemu za siri kabla ya tendo la ndoa.
6. Kuvaa nguo za ndani za pamba na zisizobana sana kuzuia sehemu za siri kupata joto kupita kiasi.
7. Kwa wanawake, haitakiwi kutumia vitu vikali au kuweka vitu vitu fulani sehemu za siri. Pia inashauriwa kubadilisha pedi mara kwa mara wakati wa hedhi pamoja na kunawa na maji safi na salama tu bila kuzuia michubuko sehemu za siri!

0 comments