Chamacha Walimu Tanzania (CWT), kimeanza kuibip serikali ya Rais John Magufuli kwa kuitaka a iwe imelipa madai yao kabla maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi) mwaka huu ili kuepusha sherehe hizo kuingia doa.
Rais wa CWT, Gratian Mukoba, alisema jana kuwa uamuzi huo umetokana na maazimio ya Baraza Kuu la Chama hicho, lililokaa Januari 28 hadi 30 mwaka huu mkoani Dodoma.
Alisema chama hicho kinataka kuona wanachama wake wastaafu wanalipwa mafao yao haraka na kwamba Baraza Kuu pia limeazimia pia kuwapeleka walimu wake ambao hawajapanda madaraja kwa wakurugenzi wa halmashauri ili wawape barua za kupandishwa madaraja.
Mukoba alisema anajua umuhimu wa sherehe za Mei Mosi na asingependa kuona zinakwama hasa ikizingatiwa kuwa ni sherehe za kwanza kwa Rais Magufuli, lakini ni lazima wastaafu walipwe mafao yao na walimu waliokwama kupandishwa madaraja wapandishwe.
“Sheria inasema mtu aliyecheleweshewa mafao anastahili kulipwa nyogongeza ya asilimia 15 ikiwa ni fidia ya usumbufu, hivyo tunaomba watakapowalipa wawape na hiyo nyongeza, maana wamewasumbua sana na wakaurugenzi wa manispaa nao wawape barua za kuwapandisha madaraja walimu ambao wanasotea barua hizo,” alisema Mukoba.
Mukoba alisema kuna walimu zaidi ya 200 ambao walistaafu, lakini bado wanazungushwa zungushwa kulipwa mafao yao na walimu wanaostahili kupandishwa madaraja hawajapewa barua za kwa muda mrefu, jambo linalowanyima haki.
CHANZO: NIPASHE
0 comments