Tuesday, 22 March 2016

MBUNGE VITI MAALUMU ASAIDIA AKINA MAMA WAJASILIAMALI.

By    

 Mbunge wa viti maalumu mkoa wa Iringa (ccm) Rose Tweve

 Mbunge wa viti maalumu mkoa wa Iringa (ccm) Rose Tweve akiwana baadhi ya wananchama wa chama ch mapinduzi.
Na Sebastian Emmanuel jr. Mafinga.


Mbunge wa viti maalumu mkoa wa Iringa (ccm) Rose Tweve ameendelea kukutana na makundi mbalimbali katika mkoa huo, mwishoni mwa wiki hili amekutana na wajasiliamali wanawake katika makundi mawili tofauti. Kundi la kwanza alilokutana nalo ni lile la umoja wa wanawake wa ccm Iringa mjini, waliounda vicoba kwa ajili ya kukopeshana na kuendeleza miradi kadhaa ya kijasiliamali.


Aidha wanawake hao wakati wakisoma risala kwa mbunge huyo wamesema kuwa wanakabiliana na changamoto kadhaa hasa ukosefu wa mtaji utakao wafanya waendeleze vicoba hivyo ambavyo imekuwa kimbilio la makundi mbalimbali mijini na vijijini.


Pia wanawake wao wamemwomba mbunge huyo kuhakikisha kuwa wanawake wa mkoa wa Iringa wanakuwa mfano wa kuigwa katika kuanzisha, kukilinda na kukitetea chama chao hicho cha vicoba kwa kuwa vinaonesha nia ya kuwasaidia kujikimu kimaisha, mpaka sasa wameanza kutafuta wataalamu wa kufundisha namna ya kufuga kuku ili wapate elimu sahihi na kasha kuanza kutekeleza mladi huo.



Kwa upande wake mbunge huyo kijana ametoa milioni moja taslimu kama mkopo usiokuwa na riba ili uweze kuwasaidia kuendeleza mtaji wao pia akatumia fursa hiyo kuwaomba mkopo huo wauzungushe katika miradi mbalimbali kama ya ufugaji kuku n.k. pia ameonesha nia ya kuwasaidia wanawake hao na kuwaahidi kuwa wakiwa na uaminifu wa kulinda mtaji wao hata kama ni mdogo atahakikisha kuwa vicoba hiyo inakuwa ya mfano wa kuigwa mkoani Iringa. 


Mbunge huyo amewaomba wanawake wote wa mkoa wa Iringa wasikate tamaa badala yake wapende kujifunza na kutaka kupata nafasi ambayo itawapeleka kwenye mwanga wa  mafanikio. Amesema kuwa hata yeye amekuwa akithubutu kujituma kwa bidii ili aweze kufikia lengo la kuwasaidia wanawake wote bila kujali itikadi, kabila wala dini zao.


Aidha kundi jingine la pili ni lilela wanawake wanaoishi na ulevu Mjini Iringa, wametumia fursa hiyo kuongea na mbunge huyo na kumweleza changamoto wanazokumbana nazo, ikiwa ni pamoja na kutokuwa na mtu wa kuwasaidia kwa mda mrefu kulingana na changamoto zinazo wakabili na kuonesha imani kwa mbunge huyo kuwa sasa wanamatumaini mapya kuwa wamepata mtu muafaka wa kuwasaidia.


Wanawake hao wanaoishi na ulemavu wameomba pia kupatiwa mtaji ili uweze kuwasaidia katika umoja wao wa kazi za mikono ikiwa ni ususi wa shanga za kimasai, mikoba ya kimasai na mikoba ya kisasa kwa kutumia shanga mbalimbali za asili, ambapo mbunge huyo licha ya kuwapa kiasi cha pesa kwa ajili ya kuendeleza mtaji wao pia amewaomba waanzishe mladi wa utengenezaji wa batiki utakao wanufaisha kwa kiwango kikubwa kwani unaonesha kuwa na soko la uhakika.


.

0 comments