Mkuu wa ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Zulmira Rodrigues (katikati) akifurahi jambo na Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Abdula Lutavi (aliyeipa mgongo kamera) wakati wakisubiri kumpokea mgeni rasmi Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Samia Suluhu Hassan (hayupo pichani) kwa ajili ya kufungua Kongamano la pili la kimataifa la uchumi endelevu unaozingatia uhai wa mazingira kama njia ya kupunguza umaskini, kulinda bayoanui na maendeleo endelevu Kusini mwa Jangwa la Sahara linaloendelea katika hoteli ya Tanga Beach Resort, Mkoani Tanga. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu Msaidizi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) kanda ya Afrika, Firmin Matoko. (Picha zote na Zainul Mzige wa Modewjiblog)
Kongamano la pili la kimataifa la uchumi endelevu unaozingatia uhai wa mazingira kama njia ya kupunguza umaskini, kulinda Bayoanui na maendeleo endelevu Kusini mwa Jangwa la Sahara (GEBR) limefanyika mkoani Tanga.
Wenyeji wa kongamano hilo walikuwa ni Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, sayansi na Utamaduni (UNESCO) ofisi ya Dar es salaam.
Akifungua kongamano hilo Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ameiomba Serikali ya Jamhuri ya Korea kusini kupitia shirika lake la maendeleo na ushirikiano la kimataifa (KOICA) kuongeza muda wa mkataba wa mradi wa GEBR ambao unafikia ukomo mwishoni mwa mwaka huu.
Akizungumza na washiriki mbalimbali wapatao 40 kutokana ndani na nje ya nchi zikiwemo Ghana na Nigeria kutoka Afrika, alisema ombi hilo linatokana na ukweli kuwa walengwa wamekuwa wakifaidika na mradi huo, kwa kuweza kubadilisha maisha yao na kuwa bora zaidi.
Makamu wa Rais alisema Tanzania ni miongoni mwa nchi zilizoathirika na kutoweka kwa uotoasili unaotoa fursa ya uoto wa mimea zaidi ya 10,000, jamii 6,000 ya wadudu, jamii ipatayo 1000 ya ndege warukao.
Aidha Samia katika hotuba yake alirejea msimamo wa serikali wa kutaka kuhifadhi mazingira, pamoja na kuziweka rasmi chini ya uangalizi halali jumla ya hekta milioni 33.5 za misitu asili, huku akitanabaisha kuwa serikali pia ina mapori ya akiba yapatayo 800 pamoja na misitu mingine.
Aliwakumbusha washikadau pamoja na nchi wafadhili kwamba Tanzania inakabiliwa na ukuaji mkubwa wa idadi ya watu wake wanaotegemea raslimali kwa matumizi yao ya kila siku pamoja na mahitaji ya nishati.
“Tunaelewa kwamba kuna shughuli nyingi za uharibifu wa mazingira zinazopelekea uharibifu wa misitu na mazingira”, alisema Samia na kuongeza kwamba kuna kupokonyana kwa ardhi na maji.
Katika warsha hiyo wafaidika wakubwa katika mradi huo, ambao walitekeleza kwa vitendo elimu iliyopatikana kutokana na mradi huo, walikabidhiwa vyeti ya ushiriki kwa vitendo na kwa ufanisi mkubwa walioonyesha.
Washiriki hao wengi walitoka katika miradi midogo midogo inayotekelezwa Amani, Muheza ambayo ni pamoja na ufugaji nyuki, samaki, vipepeo na uyoga.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Samia Suluhu Hassan (kushoto) akisalimiana na Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Bi. Zulmira Rodrigues (kulia) alipowasili kwenye hoteli ya Tanga Beach Resort jana kufungua Kongamano la pili la kimataifa la uchumi endelevu unaozingatia uhai wa mazingira kama njia ya kupunguza umaskini, kulinda bayoanui na maendeleo endelevu Kusini mwa Jangwa la Sahara lililoandaliwa na UNESCO. Katikati ni Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Mhandisi Ngosi Mwihava.
Awali, Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mwantumu Mahiza aliwataka wakazi wa Tanga na Tanzania kwa ujumla kutumia vyema nafasi adhimu kwenye miradi ya maendeleo inayogharimiwa na wafadhili na kuwasihi wawe makini kwani mafanikio yao huwa ni kivutio kwa wafadhili kuweza kuendelea kutoa ufadhili kwa misaada.
Mradi wa GEBR ambao uko katika mwaka wa tatu wa utekelezaji wake, unafadhiliwa na serikali ya Korea kupitia Shirika lake la Kimataifa la misaada Korea International Cooperation Agency (KOICA).
Mradi huo wa Unesco wa binadamu na bayosfia (MAB) unatekelezwa nchini Ghana, Nigeria na Tanzania kwenye milima ya Usambara.
Katika hotuba yake Mkurugenzi Mkuu msaidizi wa UNESCO kanda ya Afrika, Firmin Matoko alimpongeza Makamu wa rais kwa kuwa mwanamke wa kwanza kushika nafasi ya juu katika utawala tangu historia ya kuundwa kwa Tanzania.
Alisema amefurahishwa sana na wanawake kuchukua nafasi kwa kuwa Unesco wameweka kipaumbele wanawake katika maendeleo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Samia Suluhu Hassan akiwasili kwenye ukumbi wa mikutano hoteli ya Tanga Beach Resort akiwa ameambatana na Mkurugenzi Mkuu Msaidizi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) kanda ya Afrika, Firmin Matoko.
Akizungumzia mradi wa GEBR alisema umelenga kutekelezwa katia msingi wa wazo la UNESCO la binadamu na bayosfia.
Alisema kwamba mradi huo umelenga kutumia elimu ya asili, elimu ya sayansi na utamaduni ili kuboresha maisha ya biandamu huku wakihifadhi mazingira.
Aidha alitaka kuwapo ushirikiano katika utekelezaji wa ajenda za maendeleo na hifadhi ya bayosfia kwa lengo la kuwezesha maendeleo endelevu.
Washiriki wa mradi huo pia walipata nafasi ya kutembelea eneo la hifadhi ya Usambara mashariki.
Naye Balozi wa Jamhuri ya Korea, Bw Geum-Young Song alisema kwamba wataendelea kushiriki katika mradi huo ambao umejikita katika kuwezesha maendeleo endelevu huku mazingira yakihifadhiwa.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Maimuna Tarishi akizungumza machache kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kufungua Kongamano la pili la Kimataifa linayojadili kuhusu Bayoanuai katika hifadhi ya kupunguza umaskini na uhifadhi ya viumbe hai na maendeleo endelevu kusini mwa Jangwa la Sahara. Kongamano hilo limefunguliwa Februari 29, 2016 katika ukumbi wa Hoteli ya Tanga Beach Resort Mkoani Tanga.
Alisema ni lengo la taifa lake la kuwezesha hifadhi endelevu kwa maendeleo endelevu.
Aidha alitaka kuwepo na fikra za mradi kuwa endelevu baada ya wafadhili kuondoka.
Viongozi waliohudhuria siku ya ufunguzi ni pamoja na Makamu wa Rais Tanzania, Mh. Samia Suluhu Hassan, Mkurugenzi Mkuu msaidizi wa UNESCO kanda ya Afrika, Bw. Firmin Matoko, Balozi wa Jamhuri ya Korea nchini Tanzania, Mh. Geum -Young Song, Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Unesco nchini Tanzania, Zulmira Rodrigues, Wawakilishi wa KOICA nchini Ghana, Nigeria na Tanzania; mwakilishi wa KOICA nchini Korea, Seoul; na kamati za MAB kutoka nchi zinazotekeleza mradi huo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akifungua Kongamano la pili la Kimataifa linayojadili kuhusu Bayoanuwai katika hifadhi ya kupunguza umaskini na uhifadhi ya viumbe hai na maendeleo endelevu kusini mwa Jangwa la Sahara. Kongamano hilo limefunguliwa Februari 29, 2016 katika ukumbi wa Hoteli ya Tanga Beach Resort Mkoani Tanga.
Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Bi. Zulmira Rodrigues akizungumza machache kabla ya kumkaribisha Mkurugenzi Mkuu Msaidizi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Afrika, Firmin Matoko kuhutubia kwenye kongamano hilo.
Mkurugenzi Mkuu Msaidizi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) kanda ya Afrika, Firmin Matoko akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la UNESCO, Irina Bokova wakati wa ufunguzi wa Kongamano la pili la kimataifa la uchumi endelevu unaozingatia uhai wa mazingira kama njia ya kupunguza umaskini, kulinda bayoanui na maendeleo endelevu Kusini mwa Jangwa la Sahara linaloendelea katika hoteli ya Tanga Beach Resort Mkoani Tanga.
Balozi wa Jamhuri ya Korea nchini, Mh. Geum-Young Song ambao ni wafadhili wa mradi wa uchumi wa kijani kwa kulinda bayoanui akisoma taarifa yake baada ya mgeni rasmi Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, kufungua Kongamano hilo la pili la Kimataifa inayojadili kuhusu Bayoanuai katika hifadhi ya kupunguza umaskini na uhifadhi ya viumbe hai na maendeleo endelevu kusini mwa Jangwa la Sahara. Warsha hiyo imefunguliwa Februari 29, 2016 katika ukumbi wa Hoteli ya Tanga Beach Resort Mkoani Tanga.
Pichani juu na chini washiriki wa Kongamano la pili la kimataifa la uchumi endelevu unaozingatia uhai wa mazingira kama njia ya kupunguza umaskini, kulinda Bayoanui na maendeleo endelevu Kusini mwa Jangwa la Sahara linaloendelea katika ukumbi wa Hoteli ya Tanga Beach Resort Mkoani Tanga.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi cheti Mwenyekiti wa Chama cha Wakulima wa Uyoga (DMGA), Bi Judith Simon Muro, kwa kutambua mchango na ushiriki wao kwenye kutekeleza mradi wa uchumi wa kijani kwa kulinda bayoanui.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi cheti Mhifadhi wa Hifadhi ya Mazingira asili Amani (Amani Forest Nature Reserve - ANR), Bi. Mwanaidi Kijazi, kwa kutambua mchango na ushiriki wao kwenye kutekeleza mradi wa uchumi wa kijani kwa kulinda Bayoanui. Wanaoshuhudia tukio hilo kulia Mkurugenzi Mkuu Msaidizi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) kanda ya Afrika, Firmin Matoko, Balozi wa Jamhuri ya Korea nchini, Mh. Geum-Young Song (wa pili kushoto) pamoja na Mkurugenzi wa Shirika la Kazi Ofisi ya Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi, Bi. Mary Kawar (wa kwanza kushoto).
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi cheti Amiri Saidi Sheghembe wa mradi wa Vipepeo Amani kwa kutambua mchango na ushiriki wao kwenye kutekeleza mradi wa uchumi wa kijani kwa kulinda Bayoanui.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Samia Suluhu Hassan , akifurahi jambo na Mkurugenzi wa Shirika la Kazi Ofisi ya Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi, Bi. Mary Kawar.
Mgeni rasmi Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Samia Suluhu Hassan katika picha ya pamoja na washiriki kutoka nje ya Tanzania wanaohudhuria Kongamano la pili la kimataifa la uchumi endelevu unaozingatia uhai wa mazingira kama njia ya kupunguza umaskini, kulinda bayoanui na maendeleo endelevu Kusini mwa Jangwa la Sahara linaloendelea katika hoteli ya Tanga Beach Resort.
Mgeni rasmi Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Samia Suluhu Hassan katika picha ya pamoja na washiriki wa Kongamano la pili la kimataifa la uchumi endelevu unaozingatia uhai wa mazingira kama njia ya kupunguza umaskini, kulinda bayoanui na maendeleo endelevu Kusini mwa Jangwa la Sahara linaloendelea katika hoteli ya Tanga Beach Resort.
Mgeni rasmi Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Samia Suluhu Hassan katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa UNESCO walioshiriki kwenye maandalizi ya kongamano hilo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Samia Suluhu Hassan akiteta jambo na Afisa Tathimini na Logistki wa UNESCO Ofisi ya Dar es Salaam, Rahma Islem (kulia) mara baada ya zoezi la picha ya pamoja.
Mkurugenzi Mkuu Msaidizi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) kanda ya Afrika, Firmin Matoko (kushoto) akisalimiana na mmoja wadau wa maendeleo Balozi wa Jamhuri ya Korea nchini, Mh. Geum-Young Song .
Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Maimuna Tarishi katika picha ya kumbukumbu na Mwanafunzi wa kidato cha pili ambaye pia ni Katibu Klabu ya Safe Space inayojihusisha na utunzaji wa Mazingira, Lilian Tadei wa Shule ya Sekondari Potwe, Muheza.
Mkuu wa ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Zulmira Rodrigues (katikati) akiwa kwenye picha ya kumbukumbu na Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Maimuna Tarishi (kushoto) na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Mhandisi Ngosi Mwihava.
0 comments