Thursday 26 May 2016

MAONYESHO YA BIDHAA ZA PLASTIKI, MPIRA, KEMIKALI ZA PETROLI NA UJENZI KUFANYIKA MEI 27-29 MLIMANI CITY JIJINI DAR ES SALAAM

By    
Meneja Mkuu wa Expo One,  Ahmed Barakat, akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo jioni kuhusu maonyesho hayo.
Balozi wa Tanzania nchini Misri, Balozi Hamza Mohamed Hamza akizungumza katika mkutano huo.
Taswira meza kuu.
Wadau wakiwa kwenye mkutano huo.
Mwenyekiti wa Africa-PPB Tanzania, Mohamed Sami akizungumza katika mkutano huo.
Mkutano ukiendelea.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
Khaled Abu El M karem akizungumza kwenye mkutano huo.
Na Doto Mwaibale

TANZANIA inatarajiwa kuwa mwenyeji wa maonesho ya kwanza  ya bidhaa za plastiki, mpira, kemikali za petrol na ujenzi  yanayotarajiwa kufanyika katika  Mei 27 hadi 29 mwaka huu katika ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha Mlimani City jijiniDare s Salaam.

Akizungumza jijini Dar es Salaam leo, Meneja Mkuu wa Expo One,  Ahmed Barakat,  alisema nchi zote za Afrika Mashariki na kati zitashiriki katika maonesho hayo.

Alisema Maonesho ya Afrika –PPB-EXPRO yatakuwa ni jukwaa la kipekee la bidhaa mpya  na yatatoa mwanya wa kuyaelewa  masoko yake ambayo hayafahamiki vizuri.

 “Maonesho haya yamebuniwa kwa lengo la  kukuza umoja miongoni mwa Waafrika kwa kuimarisha mahusiano ya kibiashara  kati ya Misri na Tanzania na hali kadhalika  kuyaweka masoko yake kwenye ramani ya Afrika,kubainisha  kuwa Tanzania ni ya kwanza  katika orodha ya nchi za Afrika ambapo Africa-PBB-EXPO imepanga kushirikiana nayo.

“Aramex Africa ni mshirika rasmi wa usafirishaji wa Africa-PBB-EXPO na itakwua inatoa mchango mkubwa katika kutoa huduma za ugavi na usafirishaji  kutoka Misri hadi Tanzania,” alisema.

Alisema kupitia Aramex na kwa uratibu wa TanTrade na Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Africa-PBB-EXPO  inatoa fursa ya kipekee kwa waoneshaji  walio na kanzidata za kina kusajiliwa mara zinapopokelewa.

Alieleza kwamba kanzidata hizo zinajumuisha hali ilivyo ndani ya soko la Tanzania na thamani yake pamoja na takwimu sahihi ya kuuza na kuagiza, hii inatoa  fursa ya uhakika kwa mikutano ya mkakati ya B2B pamoja na ufanisi unaohusiana pindi zinapofika.

Barakat alitoa wito kwa wafanyabiashara kushiriki katika maonesho hayo ili kuweza  ‘kubaini fursa za ushirikiano katika masoko haya mapya pamoja na mtandao ulio na wateja na wenza wa kibiashara. 

“Kwa kushiriki katika maonesho ya Africa-PPB-EXPO, pamoja na mambo mengine washiriki watajifunza jinsi maudhui ya kina ya sekta yanaweza kuathiri biashara zao,  umoja uliopo miongoni mwa viongozi wa sekta, kupata washirika wapya na kulinganisha kiwango chao katika mitazamo ya ubunifu.

“Kampuni ya EXPO ONE ambayo ni mwandaaji, ni taasisi ya kati ya  usimamizi wa mikutano na maonesho ambayo imejikita katika  kuandaa na kutoa huduma kwa maonesho ya  biashara ya kimataifa  pamoja na 
kuyatangaza mabanda ya Misri katika maonesho ya ndani na ya kimataifa.
 Alisema kwamba maonesho mengine  ya Africa-PPB-EXPO yanatarajiwa kufanyika nchini Senegal na baadaye nchini Angola.



0 comments