Dar es Salaam Julai 13,
2016-kampuni
inayoongoza kwa mtindo wa maisha ya kidijitali Tigo Tanzania leo imeingia ubia
na Wizara ya Mawasiliano, Ujenzi na Miundombinu katika kuwezesha kufikiwa kwa
intaneti katika shule za sekondari nchini
ili kuwezesha elimu kielektroniki shuleni katika zoezi ambalo litachukua miaka miwili.
Kama sehemu ya makubaliano hayo,
wizara itabainisha na kutoa orodha ya
shule zisizo na maabara za kompyuta ili ziunganishwe na hali
kadhalika kuongoza utekelezaji wa
mradi wakati Tigo itadhamini maendeleo
ya miundombinu katika shule nchini ikiwa ni pamoja na kuunganisha nyaya ndani
ya madarasa na kufunga visivyotumia
nyaya (LAN) na vituo vinavyofikia
mtandao wa intaneti.
Alipokuwa akisaini makubaliano hayo katika
Shule ya Sekondari Jangwani jijini Dar es Salaam, Ofisa Mkuu wa Biashara wa
Tigo, Shavkat Berdiev, alisema, “Kupitia Idara yetu ya huduma kwa jamii hivi
sasa tunatekeleza dira ya serikali ya kuibadilisha nchi kuingia katika uchumi
uliojikita katika uelewa ifikapo mwaka 2025 na kampuni yetu imejipanga kuhakikisha shule nyingi za sekondari Tanzania zinafikiwa na mtandao wa intaneti.
“Tunajivunia
kushirikiana na Wizara ya mawasiliano, Ujenzi na Miundombinu katika kuwezesha vijana na jamii kwa ujumla kuingia katika mkondo wa kidunia wa habari na uelewa, ambako watajifunza, kupanua uelewa
wao na kushirikiana na wenzao katika sehemu mbalimbali duniani.”
Berdiev aliongeza kusema, “Tigo
itaendelea kufanya kazi na serikali katika miradi
mingine ya ubunifu na inayovutia ili kunyanyua maisha ya Watanzania
walio wengi”.
Akiishukuru Tigo wakati wa kusaini
makubaliano hayo Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano, Ujenzi na Miundombinu
Pro. Faustine Kamuzora alisema, “Ni kupitia ushirikiano kama huu ndipo tutaweza
kusambaza stadi za kisasa za Tehama pamoja na uelewa kwa vijana ili
kuwawezesha kukabiliana na
changamoto zinazotokana na mtiririko wa
mabadiliko ya habari ya kila siku ndani ya jamii na katika uchumi wa dunia.”
Prof. Kamuzora aliongeza, “Naipongeza
Tigo kwa utayari wake wa kujingiza katika makubaliano baina ya sekta binafasi
na sekta za umma ili kuwasaidia wanafunzi wa shule za sekondari nchini Tanzania
na vile vile tunakaribisha wadau wengine
kushiriki kuunganishwa kwa teknolojia hii.
Mradi wa kielektroniki mashuleni
(eSchools) ni moja ya miradi mkakati ya uwekezaji kijamii ya Tigo na hadi sasa
Tigo imeweza kuunganisha shule 31 za sekondari za serikali na
mtandao wa intaneti ikiwa na mpango wa baadaye wa kuziunganisha shule 50 kwa mwaka huu.
|
0 comments