Jumapili ya juni 16 katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, kunatarajiwa kuwekwa historia mpya katika medali ya soka la hapa nchini pale timu ya taifa Taifa stars itakapo wa karibisha Ivory coast, mchezo wa tano wa kusbka nafasi ya kucheza kombe la dunia nchini Brazil.
Mchezo huo utakao anza saa 9 kamili alasiri utachezeshwa na mwamuzi toka Algeria, ambapo viingilio ni vile vile vya michezo inayochezwa katika uwanja huo ambapo kiingilio cha chini ni 5000.
Taifa stars chini ya Kim Poulsein aijapoteza mchezo wowote ule katika uwanja wa Taifa ambapo amesha cheza na Zambia, Cameroun na Malawi ambapo ametoa sare na Malawi ya bila kufungana na kuwakishinda dhidi ya Zambia na Cameroun katika michezo ya kirafiki.
Taifa stars katika uwanja wa Taifa wamewafunga Morocco na Gambia katika michezo ya kusaka tiketi ya kushiriki kombe la dunia mwakani, na jumapili hii wanaitimisha michezo ya nyumbani, katika utafutaji wa tiketi ya kwenda nchini Brazil.
Taifa star wakifanikiwa kuwafunga Ivory coast watakuwa wamefufua matumaini ya kwenda Brazil, huku wakiwa historia ya kufanikiwa kuchukuwa point zote za michezo ya nyumbani, katika michezo ya kusaka nbfasi ya kombe la dunia na hata mataifa huru ya Afrika.
Tukiungana kwa pamoja sababu ya kuwafunga miamba hiyo ya Afrika tunayo, kwa pamoja twenzetu Brazill
0 comments