Saturday 15 June 2013

SAMATA KIBOKO MAZEMBE

SAMATTA remains the key man
Kwa mujibu wa takwimu zilizotlewa na klabu ya TP Mazembe. kwa kutumia
vigezo vya: Kucheza mechi, Pasi zilizozaa matunda na Mabao -
mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania anayekipiga kwenye klabu hiyo
Ally Mbwana Samatta ameongoza kwa kipindi cha takribani miezi 2, April
na May.

MECHI/MUDA WALIOCHEZA
Kwa kuzingatia muda wa kucheza, hakuna aliyeweza kutimiza michezo 13
ndani ya kipindi cha miezi miwili. Mwezi May wachezaji wengi wa kikosi
cha kwanza walicheza mechi zote saba, wakati katika kuleta utofauti
KASUSULA na SAMATTA walicheza mechi zote sita. Katika dakika
walizocheza Samata tayari alikuwa anashika nafasi ya 3 nyuma ya
Richard KISSI Boateng na Kasongo Kabiona.
Dakika walizocheza kwa namba: 1. KIDIABA na KASUSULA dakika 900.
3. SAMATTA 873
4. BOATENG 79
5. KABIONA 720
6. SINKALA 655
7. KIMWAKI na HICHANI 630
9. MPUTU 610
10. ASANTE 518
11. KALABA 512
12. ILONGO 475, 13. NKULUKUTA 447, 14. KABANGU 430, etc.

Mabao - Samatta anaongoza
Hakuna shabiki yoyte wa TPM anayeweza kushangazwa na mshambuliaji huyu
wa kibongo kushika nafasi ya kwanza. SAMATTA amefunga mabao 6 ndani ya
miezi mwili, akifuatiwa na Bokanga aliyefunga 5, Awako na Tresor Mputu
wamefunga mabao 4 kila mmoja huku mshambuliaji mwingine wa kibongo
Thomas Ulimwengu akifunga mabao 2.

Pasi za mabao: MPUTU anaongoza ...
Tresor MPUTU ameendelea kuwa mfalme wa pasi za mwisho ndani ya TP
Mazembe. Lakini Samata hayupo mbali - anashika nafasi ya pili.
Waliongoza: 1. MPUTU pasi 6 , 2. SAMATTA pasi 5,
3. BOATENG 2, 6. ASANTE, BOKANGA, KABANGU, KASONDE, ADJEI, NKULUKUTA,
ULIMWENGU kila mmoja alitoa pasi 1 ya goli.



KITAA: SHAFFIH DAUDA BLOG

0 comments