Sunday 16 June 2013

TUNAWEZA BILA YA KAMATI

Taifa stars iliyoikabili Ivory coast
Na Abdallah H.I Sulayman, Sport In Bongo

Habari za sa hizi wapenzi wasomaji wa blog hii na ninaanza kwa kuwapongeza wachezaji wa stars kwa kazi nzuri waliyoifanya hii leo (juni16) japo kuwa wamepoteza mchezo dhidi ya Ivory coast na kupelekea kuendelea kuqwa watazamaji wa michuano ya kombe la Dunia kama ilivyo ada yetu.

Sito zungumzia namna stars walivyo fikia hapo walipo, bali nitagusia suala la kamati ya ushindi  ambayo hujitokeza pale dira fulani inapoanza kuchomoza katika timu zetu za Taifa katika michuano ya kusaka nafasi ya kushiriki michuano mbalimbali.

Kuhamasiha si kosa na hamasa inahitajika katika mbio za kusaka nafasi ya kushiriki michuano mikbwa Duniani kama ili ya kombe la Dunia, Olimpik, kombe la mataifa ya Afrika nakadhalika.

Huhamisishaji hufanywa kwa mashabiki ili waweze kujitokeza kwa wingi uwanjani kuiunga mkono timu ya taifa sambamba na kuwapa ahadi mbalimbali wachezaji na benchi zima la ufundi. Kazi hiyo kubwa hufanywa na kamati hizo za ushindi.

NYAKATI ZINAPO UNDWA


Wakati harakati ya kusaka tiketi ya kombe la Dunia zinaanza haikusikika kamati yoyote ile, ila iliundwa baada ya TAifa stars kufikisha point 6 baada ya kuwafunga Moroco na Gambia katika uwanja wa taifa ndipo ilipokuja kuundwaq kamati ya ushindi.

Mara zote kamati za ushindi huundwa wakati teyarik unamatumaini fulani, kama hiyo ya kusaka nafasi ya kwenda Brazili, ukirudi nyuma kamati ilipata kuundwa ya kuhakikisha timu ya vijana chini ya mika 17n wanakata tiketi ya kushiriki mashindano ya Afrika kwa vijana wenye umri huu wakati timu teyari ipo katika hatua ya mwisho ya kusaka nafasi hiyo.

Hizo ni mifano ya kamati inayo undwa kwa malengo ya kuwapa hamsa zaidi wachezaji na kuwahamsisha mashabiki wajitokeze kwa wingi.

AHADI KWA WACHEZAJI 

Kamati zote zinazo undwa huishia kutoa ahadi mbalimbali ambazo mpaka sasa ajapata kusikika manunguniko ya kuto patiwa ahadi wanazo ahidiwa pale mabo yanapo kwenda sawa.

Ahadi imekuwa ikitumika kama chachu ya kuwafanya wachezaji waongeze juhudi katika mchezo usika katika bara letu la Afrika mabapo mara nyingi hutolewa katika mazingira ambay timu ni ngumu kupata matokeo.

Taifa stars wali ahidiwa zawadi nono kama wangepata matokeo nchini Moroco, ambapo mara nyingi kama si zote Taifa stars hawakufanikiwa kupata matokeo katika ardhi ya Waarabu wa Afrika (Tunisia, Algeria, Misri).

Ni mara chache hutokea timu ya taifa ikiahidiwa kitu baada ya matokeo fulani kutokea. Ahadi hutolewa kabla ya mchezo tena mchezo ambao Stars wana asilimia chache za kupata angalau sare.

NI IPI TIJA YA KAMATI

Kamati zetu za ushindi hazina tija na wala hazitatupeleka kokote kule bila ya kuweka mipango endelefu ya michezo nnchini na wala si kukurupuka na kutaka kujizolea sifa katika mgongo wa mtu.

Ninge utambua umuhimu wa kamati kama inaanzia mwanzo wa kampeni ya kusaka nafasi wala sio katikati ya kampeni za kusaka tiketi ya kushiriki michuano husika.

Kamati hazichezi mpira, wanao cheza ni wachezaji, asmbao bila ya kuwajenga vizuri kamwe ata uwaaahidi kiasi chochote cha fedha kamwe hawataweza kufikia azima iliyo nayo kamati.

Kama kweli tunahitaji maendeleo katika michezo lazima kwanza tuweke misingi sawa ya michezo hiyo kabla ya kukimbilia kwenye kamti.

Leo Stars walikuwa na uwezo wa kushinda magoli zaid ya matatu troka kwenye mibira ya adhabu na kona walizo pata, lakini kutokana na kutoandaliwa vyema wamekuta wakiziacha ahadi walizotolewa zipite.

HITIMISHO

Kamati bila mipango endelevu ya kuendeleza mchezo husika ni kazi bure. Kitangulie mipango endelevu kisha kamati hizo ndizo zije. tuache kuendesha michezo kisiasa.

0 comments