TANZANIA imetakiwa kuacha tabia ya kufungia vyombo vya habari na badala yake kuvijengea mazingira mazuri ya uhuru wa habari.
Agizo hilo lilitolewa na mashirika ya kutetea haki za binadamu katika nchi za Afrika zaidi ya 200, yaliyokutana katika mji wa Banjul, Gambia katika mkutano wao wa 54 hivi karibuni.
Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa juzi na Mratibu wa Mtandao wa Kutetea Haki za Binadamu (THRD-Coalition), Onesmo Olengurumwa, ilieleza kuwa agizo hilo ni kati ya maazimio mawili kuhusu uhuru wa habari ambapo mashirika hayo yametoa azimio kwa Tume ya Afrika ya Haki za Binadamu kwa kuwataka wanachama wake kuacha kufungia magazeti.
Alisema azimio jingine limewahusu watetezi wa haki za binadamu ambao wamesisitiza mataifa yaanze kurekebisha mifumo ya sheria na kuwatambua watetezi hao ili kupunguza matukio ya kiusalama dhidi yao.
Pia alieleza kuwa Tanzania imetakiwa kufanyia kazi kesi mbalimbali kama za utesaji na unyanyasaji, kama ile ya kuteswa kwa Dk. Steven Ulimboka na kuuawa kwa mwandishi wa kituo cha televisheni cha Channel Ten, Daudi Mwangosi na kuhakikisha wahusika wote wanachukuliwa hatua.
Alieleza kwa upande wa Tanzania mashirika yaliyoshiriki mkutano huo ni mtandao wa kutetea albino nchini - Under the Same Sun, mtandao wa kutetea wafugaji uliopo Morogoro na Kituo cha Haki za Binadamu (LHRC).
CHANZO: TANZANIA DAIMA

0 comments