Imamu mkuu wa chuo kikuu cha kiislamu nchini Misri cha Al Azhar amealikwa katika kuzungumza katika sherehe za ufunguzi wa mashindano ya mpira wa miguu ya kombe la Dunia la mwaka 2014 nchini Brazil yanayotarajiwa kuanza juni mwaka huu.
Sheikh Ahmed el- Tayeb amepewa mualiko huo na balozi wa Brazil Marco Brandão nchini Misri.
Mohammad Mehanna mshauri mkuu wa Imamu aliiambia Cairo Post kwamba mualiko huo unamaanisha dhana ya utambulisho na umuhimu wa chuo cha Al Azhar ulimwenguni.
Aliongeza kusema kuwa mualiko huo utatoa fursa ya kuutangaza na kuujua uislamu kupitia hotuba ya Imamu mkuu kwani tukio la ufunguzi wa mashindano hayo huangaliwa na mamilioni ya watu duniani kote.
Mwaliko huo umekuja mwezi mmoja baada ya taarifa ya FIFA kutangaza kuwa hakutakuwa na hotuba zozote wakati wa sherehe za ufunguzi wa Kombe la Dunia mwezi Juni.
Mwaka jana, Rais wa Brazil Dilma Rousseff wakati akihutubia katika ufunguzi wa kombe la shirikisho la mabara nchini Brazil mashabiki walikuwa wakimcheka na kumzomea.
Uislamu unahimiza waumini kufanya mazoezi kwa ajili ya kuweka sawa miili na kuimarisha afya zao.

0 comments