Gazeti la Daily Mail limeripoti kuwa mfungaji bora huyu wa EPL msimu uliopita anatarajiwa kuigharimu Barcelona pauni milioni 80, kukamilisha uhamisho wake ndani ya saa 48 xijazo.
Wakati Liverpool wakijianda kumpoteza Suarez, Liverpool Echo inaripoti kuwa ofa waiyo itoa Liverpool kwa Southampton imekataliwa.
Liverpool ilitenga pauni mlioni 20 kwa ajili ya kumnasa beki wa Southampton Dejan Lovren ambalo limekataliwa.
Vilevile Daily star imeripoti kuwa Real madrid wamemuachia Angel Di Maria ajiunge na Manchester United kwa pauni milioni 40. Di Maria anatakiwa pia na Arsenal, Paris St-Germain na Juventus.
Daily Mirror nayo inaripoti kuwa meneja wa Arsenal, Arsene Wenger ana uhakika wa kuwasajili Alexis Sanchez na Mathieu Debuchy kwa pauni milioni 35.
TETESI NYINGINEZO
a. Arsenal watatoa dau la pauni milioni 20 kwa Southampton kumsajili Morgan Schneiderlin, ambaye anasakwa pia na Napoli (Daily Express).b. Bayern Munich huenda wakawazidi kete Manchester United, Liverpool na Arsenal kumchukua winga wa Fiorentina, Juan Cuadrado (Daily Express).
c. Arsenal wametoa dau la pauni milioni 23.8 kumwania kiungo wa Real Madrid, Sami Khedira na watamtumia rafiki wake wa karibu Mesut Ozil kumshawishi (Metro).
d. Dau la pauni milioni 32 la Manchester City kumtaka beki Eliaquim Mangala limekubaliwa na Porto, lakini bado wanasubiri kama Chelsea nao pia watapanda dau (Daily Star).
e. Juventus wako makini kumsajili beki wa Manchester United Patrice Evra, ambaye amesaini mkataba mpya Old Trafford mwezi uliopita (Talksport).
f. Barcelona wataajiri mwanasaikolojia wa kumsaidia Luis Suarez kukabiliana na 'mizimu' atakapokamilisha uhamisho wake (Sun)
g. QPR wanatarajia kukamilisha usajili wa Rio Ferdinand wiki ijayo (GetWestLondon), na kipa wa Chelsea Petr Cech huenda akaondoka Darajani kabla ya msimu mpya kuanza, kwa mujibu wa wakala wake (Talksport)
0 comments