Friday, 4 July 2014

UTATU WAENDELEA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI

 Marais wa Rwanda, Kenya, na Uganda wametia saini makubaliano kwenye miradi ya mkondo wa kaskazini ama norther Corridor huku Tanzania ikiwa imetengwa.


Huu ni mwendelezo wa mikutano ya awali miongoni mwa marais hao ambayo wamekuwa wakitia saini kwa ajili ya ushirikiano wa kiuchumi na ulinzi.


Miradi mikubwa ambayo inaendelea miongoni mwa nchi tatu ni pamoja na ujenzi wa reli kutoka Mombasa hadi Kigali kupitia Kampala huku sehemu moja ya reli hiyo ikielekea Juba Sudan Kusini.

 Miradi mingine ni pamoja na bomba la mafuta kutoka Kenya hadi Rwanda, pamoja na miundo mbinu kubwa inayounganisha mataifa hayo.

 Hivi karibuni nchi tatu zilikubaliana mkataba kuweka himaya moja ya ulinzi ambapo umekwishawekwa utaratibu wa kuunda kikosi maalum kwa kila nchi ambacho kitaingilia kati wakati nchi moja itakapohitaji msaada kutoka nchi ya pili.


Mwezi wa kwanza mwaka huu nchi hizo tatu zilianzisha mfumo wa kusafiri kwa wananchi wao kwa kutumia vitambulisho vya kawaida badala ya pasi za kusafiria. 

0 comments