Meneja wa Brazil Luiz Filipe Scolari amesema Neymar atakosa mchezo wa nusu fainali dhidi ya Ujerumani baada ya kuumia mgongo kwenye mchezo wa robo fainali dhidi ya Colombia.
Neymar aligongana na Juan Camilo Zuniga wa Colombia katika dakika za mwisho katika mchezo ambao Brazil ilishinda goli 2-1 na kukata tiketi ya kutinga nusu fainali ambapo watakabiliana na Ujerumani.
Neymar anaungana na nahodha wa timu hiyo Thiago Silva ambaye naye ataukosa mchezo wa nusu fainali baada ya kupata kadi ya pili ya njano katika michezo tofauti hapo jana.
Thiago Silva alionyeshwa kadi hiyo ya njano baada ya kumuingilia kipa wa Colombia wakati akitaka kuupiga mpira.
0 comments