Afisa Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa Bi. Usia Nkhoma Ledama, akizungumza na wanafunzi wa shule ya sekondari Jangwani akiwa ameambatana na maafisa wenzake wa mashirika ya Umoja wa Mataifa ikiwa ni shamrashamra ya maadhimisho ya miaka 69 toka Umoja wa Mataifa unazishwe. Kushoto kwa Bi Ledama ni Albert Okal (ILO).
Shamrashamra za maadhimisho ya miaka 69 toka Umoja wa Mataifa uanzishwe zimeanza nchini, na leo jumatano maofisa waandamizi wa UN walitembelea shule ya sekondari ya Jangwani na kuwahabarisha wanafunzi hao juu ya shughuli za Umoja wa Mataifa hapa nchini.
Mjadala kati ya maofisa hao Phillemon Mutashubirwa, Programme Manager wa UN Habitat, Usia Nkhoma Ledama, Afisa habari wa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa(UNIC), Albert Okal (ILO),Greta Sayungi (UNICEF), ulijikita katika masuala ya HIV/AIDS, EBOLA, Usafi na umuhimu wakuosha mikono ili kujikinga na maradhi, elimu ya ujasiriamali, ajira kwa vijana, kazi za kujitolea, malengo ya Milenia na malengo ya Umoja wa Mataifa kwa ujumla wake.
Ijumaa wiki hii Umoja wa Mataifa utaadhimisha mkiaka 69 toka uanzishwe na kilele cha maadhimisho hayo yatafanyika katika viwanja vya Karimjee, jijini Dar es Salaam.
Afisa Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa Bi. Usia Nkhoma Ledama akifafanua jambo wakati akizungumza na wanafunzi wa shule yasekondari Jangwani jijini Dar. Kutoka kushoto ni Phillemon Mutashubirwa (UN Habitat), Greta Sayungi (UNICEF) pamoja na Dr Bwijo Bijo (UNDP)
Pichani juu na chini ni Baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari Jangwani wakiwasiliza maafisa wa Umoja wa Mataifa waliowatembelea shuleni hapo.
0 comments