Tukio hilo la kukamatwa na kuuawa kwa majambazi hao lilitokea Julai 17 mwaka huu huko maeneo ya Tuangoma Kigamboni jijini Dar es Salaam, na majambazi wa tukio la kinyama la kuuwawa kwa askari wanne na raia watatu katika kituo cha Stakishari wanakadiriwa kuwa kati ya 16 hadi 18.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam,Kamishina Suleiman Kova amesema kukamatwa kwa majambazi hao inatokana na kikosi kazi kilichoundwa na kanda maalumu kwa kushirikia na Mkoa Pwani.
Kukamatwa kwa watuhumiwa hao wa ujambazi kulitokana na taarifa pamoja na mtego wa kiintelejensia katika eneo la Tuangoma ndipo majambazi wakapita na pikipiki mbili walipowasimamisha askari majambazi hao walikaidi amri nakisha kuanza kurusha risasi na polisi wakajibu na majambazi watatu kuuwawa.
Kamanda Kova amesema wanaowashikiria ni Ramadhan Ulatule (15),Mkazi wa Mandimkongo, Mkuranga, Omary Amour( 24) Mkazi Mkazi wa Mbagala Kimbangulile.
Kova amesema baada ya kuwabana watuhumiwa wa ujambazi walikwenda kuonyesha bunduki 15 walizopora katika kituo cha Stakishari ambazo walikuwa wamehifadhi chini ya ardhi kuweka kinyesi juu.
Amesema katika Shimo walilohifadhi walikuta bunduki aina Norinko ambayo wanatafuta ilipoibiwa pamoja na kukuta fedha taslimu Sh.Milioni 170 za kitanzania.
Aidha amesema jeshi la polisi limejizatiti katika matukio na kutaka watu waachane na biashara hiyo ya ujambazi kuwa halipi.
Amesema fedha hizo wanazichunguza kujua zimeibwa wapi,na pikipiki mbili aina ya boxer nazo wanazishiria na kutaka wauza pikipiki kuuzia watu ambao wanataarifa nazo.
“Hatutafumbia macho kwa wale askari wanaojihusisha na vitendo vya kihalifu kwa kuwachukulia hatua kali ikiwa hata kama wanajihusiha na ujambazi tutawashughulikia kwani risasi haichagui kuwa huyu raia au askari”amesema Kamishina Kova.
Tukio la kuawawa kwa askari wanne na raia watatu katika kituo cha Stakishari,lilitokea julai 12 majira ya saa nne.
0 comments