MAZOEZI ya kumsaka mlimbwende wa Tabata, 'Miss Tabata 2016', yanatarajia kuanza Jumanne ijayo kwenye Ukumbi wa Da West Park, Tabata jijini Dar es Salaam.
Mratibu wa shindano hilo Joseph Kapinga alisema jana kuwa warembo wote waliojiandikisha wanatakiwa kufika mazoezini na bado fomu za ushiriki zinaendele kutolewa.
Kapinga alisema Kampuni ya Keen Arts, ambayo ni kampuni tanzu ya Bob Entertainment ndiyo iliyopewa kibali cha kuandaa shindano hilo na waratibu wa taifa wa Miss Tanzania, Kampuni ya Lino Agency.
Kapinga alisema uzinduzi rasmi wa shindano hilo utafanyika mwishoni mwa mwezi huu.“Baada ya uzinduzi washiriki watatembelea hifadhi ya Mikumi na Dar es Salaam Zoo ikiwa ni njia mojawapo ya kutangaza utalii wa ndani,” Kapinga alisema.
Aliwataka warembo wenye sifa za kushiriki shindano hilo kujitokeza na kujaza fomu zinazopatikana kwenye Ukumbi wa Da West Park na ofisi za Miss Tanzania, Mikocheni.
Miss Tabata ni miongoni mwa vituo vitatu vilizoko Kanda ya Ilala. Vingine ni Ukonga na Dar City Centre.
Tayari Kampuni ya CXC Africa, Fredito Entertainment, Saluti5 na Bob Entertainment zimekubali kudhamini shindano hilo.
Chanzo: Nipashe
0 comments