Na Mwandishi Wetu, Arusha
Mkurugenzi
wa Jiji la Arusha Bw Athuman Kihamia amekataa kamati ya watu 4 mbele ya
Baraza la madiwani wa Jiji la Arusha iliyokuwa imepangwa kwa ajili ya
kuchunguza mgogoro wa maduka hayo 396 yalipo stand ndogo Jiji la Arusha
kwa kile alichosema kuwa wananchi bado wanawatuhumu madiwani wengi kuwa
chanza cha migogoro hiyo.
Mkurugenzi
huyo amesema kuwa binafsi haoni sababu za msingi za uwepo wa kamati hiyo
badala yake ana hofu ya kuingizwa siasa katika jambo hilo.
Kuhusu
wajenzi wa vibanda vya maduka stand ndogo, mkurugenzi wa jiji la
Arusha Bw Athumani Kihamia amewataka madiwani kutokuweka maneno ya
kisiasa katika swala hilo la kimaendeleo ambapo mpaka sasa mgogoro wa
maduka hayo takribani 396 upo katika mahakama ya ardhi jiji la Arusha.
Aidha
pia mkurugenzi wa jiji la Arusha ameongeza kwa kusema kuwa mapato
makubwa ya jiji la Arusha yalikuwa yanakusanywa kupitia maduka hayo
takribani 1196 hapa jijini maduka hayo ambayo yapo maene ya Stand
ndogo,Soko kuu,Kilombero na kijenge ambapo halmashauri ilikuwa
inakusanya shilingi Bilioni 1.2 kwa mwaka kitu ambacho kwasasa ameeleza
kuwa mapato hayo yanaweeza kupungua kutoka na mgogoro wa maduka 396
yalipo maeneo ya Stand ndogo jijini Arusha na kubaki maduka 800 yanayo
tegemewa na halmashauri hiyo ya jiji la Arusha
Diwani
wa kata ya Olasiti Bw Alex Mart ameeleza kuwa katika utatuzi wa
migogoro ya wananchi inahitajika umoja na ushirikiano wa viongozi wote
kuwa kitu kimoja pasipo kujali itikadi ya vyama vyao pamoja na nyazifa
walizo nazo badala yake busara itumike katika utatuzi wa migogoro hiyo.
0 comments