Nilitamani kuvunja mihangaiko yangu na kuelekea huko Mbande lakini iliwia ngumu baada ya kucheki ratiba ya vipindi nilivyo kuwa navyo leo na hivyo kungoja kwa hamu kusikiliza japo kuona ilikuwa ngumu kutokana na mfumo mpya wa digitali nini kilichojiri huko.
Katika tembezi za ndani ya mitandao nikakutana na kauli alizo nukuliwa Raisi Kikwete leo juu ya soka letu la bongo, na kumaliza siku kwa kusikiliza kile alicho zungumza.
Kwa ufupi alizungumzia migogoro ndani ya timu kongwe za simba na yanga kiasi kwamba hawajapiga hatua kama ilivyo kwa timu changa ya azam fc iliyoanza mnamo mwaka 2004.
Mh. Kikwete aligusia suara la uundwaji wa kamati za ufundi ambazo kazi yake kubwa ni kuwarubuni wachezaji wa timu pinzani pamoja na waamuzi sambamba na kwenda kwa waganga kusaka ushindi.
Alisema pia azam si timu ndogo tena, sara ni timu kubwa anayoitazama kuleta mafanikio katika soka la bongo kupitia katika ufumo wao wa uongozi bora.
Hayo ni kwa ufupi aliyo yasema raisi Kikwete leo, kutokana na kukosa computer leo, na simu kutokuwa na uwezo wa kucopy na kupaste, hivyo waweza pata kilicho zungumzwa leo katika www.shaffihdauda.com na www.azamfc.co.tz
--
MSUNI COMPUTER SOLUTION (Tunarejesha uhai wa computer)
www.aboodmsuni21.blogspot.com/p/msuni-computer-solution_7934.html
0 comments